loader
Picha

Biashara SADC yakua kiwango kidogo

BIASHARA ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika kwa ujumla, inatajwa kukua kwa kiwango cha chini ikiliganishwa na kanda nyingine ulimwenguni.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda na Biashara katika Sekretarieti ya SADC, Calicious Tutalife amesema ikilinganishwa na kanda nyingine duniani, biashara iko chini katika SADC na Afrika.

Akieleza shughuli za kurugenzi ya maendeleo ya viwanda na biashara kwa waandishi wa habari jana Dar es Salaam, alisema thamani ya biashara ya ndani imeendelea kubaki chini kwa asilimia 22 ya biashara yote ya SADC.

Alisema kasoro hiyo ni miongoni mwa zilizobainika kupitia maadhimisho ya wiki ya viwanda yaliyohitimishwa hivi karibuni jambo ambalo ameshauri ifanyike mikakati kuondokana nazo.

Akisisitiza jumuiya kuweka kipaumbele cha biashara ndani ya ukanda, alisema pia inapaswa kutatua matatizo ya miundombinu, kupunguza vikwazo, kuboresha ubunifu na utafiti.

Amesema baraza jipya la biashara lililozinduliwa, linapaswa kushirikiana na nchi wanachama kuboresha na kuwezesha mazingira ya ushindani kwa kuhusisha ukanda, nchi na sera za ndani kiasi cha kuwezesha kuleta matokeo chanya katika maendeleo ya kiuchumi.

Amesema pia uwekezaji katika utafiti, maendeleo na ubunifu umeendelea kubaki chini huku nchi nyingi zikiwekeza chini ya asilimia moja ya pato la ndani (GDP).

“Upo umuhimu wa kuboresha mfumo wa elimu ikiwamo teknolojia mpya, kuwekeza kwenye miundombinu ya teknolojia ya habari na mawasiliano, vituo vya umahiri, ubunifu na vituo vya viwanda ili kuongeza fursa za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda,” amesema.

Alishauri kuwa pia upo umuhimu wa kusaidia fedha za kuanzisha nyenzo za kuunga mkono ubunifu na maendeleo ya teknolojia.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amesema katika kuhakikisha ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi