loader
Picha

Majeruhi wengine 6 walioungua wafariki dunia

Majeruhi sita kati ya 38 walioungua moto mjini Morogoro na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Wagonjwa hao waliungua wakati lori la mafuta lilipolipuka Agosti 10 asubuhi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema, majeruhi 17 kati ya 32 waliobaki wapo kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) na wengine 15 wapo kwenye jengo la Sewahaji wodi namba 22.

“Tunaendelea kujitahidi kuhakikisha tunatoa kila aina ya ujuzi na utaalamu tulionao kuendelea kuokoa maisha ya wenzetu walipoko ICU na wale wenzetu walioko katika wodi ya Sewahaji wodi namba 22”amesema Aligaesha.

Hospitali ya Muhimbili ilipokea majeruhi 46 walioungua wakati lori la mafuta lilipolipuka mjini Morogoro Agosti 10 asubuhi. Hadi sasa majeruhi 14 kati ya hao wamefariki dunia hivyo wamebaki 32.

Kwa mujibu wa Aligaesha, madaktari ,wauguzi na watoa huduma wengine wanajitahidi kuokoa maisha ya majeruhi waliobaki.

“Na niseme tu kazi tunaifanya, vifaa tunavyo kuhakikisha kwamba kwa kweli kila anayehitaji msaada anaweza kusaidiwa kwa wakati mwafaka…

“Wataalamu wanapigana usiku na mchana kuhakikisha kila mgonjwa yupo karibu na mtaalamu, karibu na daktari, muuguzi, mfamasia na watoa huduma wengine kuhakikisha kwamba wanawapa huduma stahiki” amesema Aligaesha.

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi