loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mhadhiri kizimbani rushwa ya ngono

MHADHIRI katika Chuo cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (68), amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya rushwa ya ngono.

Wakili wa Serikali, Vera Ndeoya amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, kuwa, Mahimbo alitenda kosa hilo Januari 12, 2017 maeneo ya nyumba ya kulala wageni ya Camp David iliyopo Mlalakuwa, Mwenge.

Ndeoya amedai kuwa mshitakiwa huyo mkazi wa Ubungo Juu, alitenda kosa hilo akiwa mwajiriwa wa NIT mhadhiri wa muda kwa muhula wa kwanza wa masomo ya Load Transport Management.

Imedaiwa mahakamani kuwa, Mahimbo aliomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi Victoria Faustine likiwa ni sharti ili amsaidie kufaulu mtihani wa somo hilo uliofanyika Januari 5, 2017.

Mshitakiwa amekana mashitaka.

Upande wa mashitaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na umeomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali.

Hakimu Shaidi amemtaka mshitakiwa awe na mdhamini mwenye barua na kitambulisho kinachotambulika na kusaini bondi ya Sh 1,000, 000.

Mshitakiwa ametimiza masharti ya dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi Septemba 17 mwaka huu.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Isdory Kitunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi