loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pengo ang’atuka Jimbo Kuu Dar

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameridhia ombi la Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo kustaafu.

Kutokana na hatua hiyo, kiongozi huyo mkuu wa kanisa hilo amemteua Askofu Mkuu Mwandamizi Yuda Thaddeus Ruwa’ichi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kuwa Askofu Mkuu wa jimbo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandaliwa na Padre Richard Mjigwa na kuchapishwa na katika wa Vatican News, Papa Francis alikubali maombi ya Pengo katika maadhimisho ya “Sherehe ya Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni, mwili na roho mnamo Agosti 2019.

Taarifa hiyo inasema kuwa, hivi karibuni, Kardinali Polycarp Pengo katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya miaka 75 tangu kuzaliwa kwake, “aliwaambia watu wa Mungu Jimbo kuu la Dar es Salaam kwamba, anasubiria wakati wowote kumtii Baba Mtakatifu Francisko atakapomwambia kupumzika katika utume wa Kiaskofu.

"Anasubiria pia kumtii Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na mapendo, wakati wowote atakapomwita na kumwambia kupumzika katika usingizi wa amani na maisha ya uzima wa milele.

Kardinali Polycarp Pengo amewaambia watu wa Mungu kwamba, kaburi lake liko pale Pugu, kwenye Kituo cha Hija, mahali ambapo wamelala mashuhuda wa imani na uinjilishaji nchini Tanzania.”

RAIS wa Urusi, Vladimir ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Vatican

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi