loader
Picha

Mume, mke kortini kughushi fomu 2,470 hati za kusafiria

WANANDOA Jasmin Ngongolo na Zakayo Mazula wamefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kughushi fomu 2,472 za kutengenezea hati za kusafi ria za Tanzania na utakatishaji wa Dola za Marekani 4000.

Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili wa Serikali, Ester Martin, alidai washitakiwa hao walitenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Januari Mosi na Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam na Johannesburg, Afrika Kusini.

Ilidaiwa katika kipindi hicho,washitakiwa hao na wengine ambao hawapo mahakamani wakisaidiana na watumishi wa umma, walijihusisha katika uhalifu wa kupangwa kwa kutengeneza fomu 2472 za kutengenezea hati za kusafiria za Tanzania. Katika mashitaka ya pili, washitakiwa hao na wengine ambao hawakuwepo mahakamani, wakiwa Afrika Kusini walighushi nyaraka hizo.

Ilidaiwa kuwa, Agosti 2 mwaka huu katika Kiwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, walikutwa wakiwa na fomu hizo zilizopatikana isivyo halali. Pia ilidaiwa, washitakiwa hao wakiwa na wengine ambao hawapo mahakamani, wakiwa kati ya Dar es Salaam na Afrika Kusini bila mamlaka walitengeza fomu hizo.

Washitakiwa hao wanadaiwa kutakatisha Dola za Marekani 4,000 walizopokea kutoka kwa Yusuph Ivere maarufu kama Kingu Kiula na kuzitumia kwa ajili ya kutengenezea nyumba yake iliyoko Salasala, na kurekebishia magari yao matatu.

Ilidaiwa walifanya hivyo kwa lengo la kuficha ukweli huku wakijua fedha hizo ni mazali ya kosa la kugushi. Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu alisema washitakiwa hawatakiwi kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina màmlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Katika hatua nyingine, mahakama hiyo imeomba hati ya kuwakamata Yusuph Ivere na Kenedy Maleko.

Upande wa mashitaka ulidai washitakiwa hao wametoroka nje ya nchi baada ya kugundua uhalifu wao umebainika na wenzao wamekamatwa, ili waweze kuunganishwa katika kesi hiyo. Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 30 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi