loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzanite Yafanya maajabu Cosafa

TANZANIA imefanikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali, lakini yale ya tanzanite yako pekee nchini na huwezi kuyakuta mahali popote duniani. Na siku zote kitu kikiwa kinapatikana sehemu chache au moja, basi hakuna ubishi kuwa kitu hicho kinatakuwa na thamani kubwa kwani kitakuwa kinatafutwa sana. Madini hayo ya tanzanite hapa nchini yanapatikana katika eneo moja la Mirerani mkoani Arusha.

TIMU YA WANAWAKE

Timu ya taifa ya soka ya wanawake kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 imepewa jina la Tanzanite na hivi karibuni ilishiriki mashindano ya Kombe la Cosafa kwa wachezaji wenye umri huo.

Tanzania, yaani timu ya Tanzanite ilishiriki michuano hiyo kama mwalikwa kwani nchi yetu iko katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki, ambao chombo chao ni Cecafa na kile cha Kusini ni Cosafa. Timu hiyo ilishiriki michuano hiyo ambayo ilifanyika Afrika Kusini na kama lilivyo jina lake, ilifanya kweli na kufanya vizuri hadi kutwaa taji la michuano hiyo kwa mwaka 2019/2020.

Katika mashindano hayo, The Tanzanite walifungwa na Zambia 2-1 katika hatua ya makundi na katika kuonesha kulipa kisasi hicho, na wenyewe Tanzanite waliifunga Zambia kwa idadi hiyo ya mabao katika fainali.

USHINDI NUSU FAINALI

Katika nusu fainali, Tanzanite iliwafunga wenyeji Afrika Kusini kwa mabao 2-0 na ushindi huo ukawafumbua macho wengi na kuanza kuifikiria Tanzanite kuweza hata kutwaa ubingwa.

Tanzanite ilionesha kiwango cha hali ya juu na kuwaondosha wenyeji katika michuano hiyo na kukata tiketi ya kukutana tena na Zambia katika fainali, kitu ambacho wengi walifikiri kuwa timu hiyo haiwezi kuiondoa Zambia. Timu hiyo ilidhihirisha kuwa ina thamani kama yalivyo madini ya tanzanite, kwani ilifanya kweli na kuiondosha Zambia katika fainali na kulitwaa taji hilo, licha ya kushiriki kama mwalikwa.

IMETUTOA KIMASOMASO

Ushindi wa Tanzanite katika michuano hiyo ya Cosafa ni faraja kubwa kwa Watanzania kwani tumechoka kuwa wasindikizaji na hivyo kutufanya kuwa na kiu ya muda mrefu ya ushidi. Hongera Tanzanite. Mafanikio hayo ya Tanzanite yawe mfano kwa timu nyingine za taifa za Tanzania kuanzia zile za vijana hadi wakubwa za wanaume na wanawake ili tuendelee kushinda siku hadi siku.

KUIUNGA MKONO TIMU

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatakiwa kuiendeleza timu hiyo kwa kuiwezesha kushiriki mashindano mengi ili izidi kukomaa na hatimaye wakati utakapofika ichukue nafasi ya timu ya taifa ya wanawake ya Twiga Stars. Na kabla ya kufika huko kuchukua nafasi ya Twiga Stars, timu hiyo ya Tanzanite inatakiwa iwezeshwe kushiriki mashindano mbalimbali ya Afrika na hata dunia na bila shaka itafanya vizuri kama itaendelezwa na kupatiwa kila kinachotakiwa.

Nchi zote zilizofanikiwa katika soka ziwe timu za taifa au klabu, msingi mkubwa wa mafanikio yao ni kupitia timu za vijana, ambayo zimeendelezwa kwa muda mrefu hadi kufikia huko zilipofikia. Tanzanite ni vijana wadogo, ambao wameonesha uwezo mkubwa na kizuri wachezaji wengi wanatoka katika timu tofauti tofauti na mikoani na hii imedhihirisha utaifa kweli kweli. Hakuna shaka kuwa Tanzanite ikiendelezwa inaweza kuifikisha mbali Tanzania katika soka la wanawake, ambalo kwa miaka kadhaa hatujapata mafanikio.

KUPANGA NI KUCHAGUA

Wakati umefika sasa wa Tanzania kuchagua tushiriki mchezo gani katika michuano ya kimataifa kwa sababu inaonekana tumeshindwa kufanya vizuri katika michezo mingine, hivyo kupanga ni kuchagua tufanye nini na kuachana na nini.

Tunaweza kuamua tukaachana na mambo mengine na kukimbilia katika soka la wanawake, ambalo inaonekama linaweza kututoa kimasomaso na kutufuta machozi ya muda mrefu baada ya kukosa mataji ya kimataifa kwa miaka mingi.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi