loader
Picha

Simba, Azam hapatoshi leo

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wametamba kutetea Ngao ya Jamii leo wakati wakapokutana na Azam FC, licha ya kuwakosa wachezaji wake watatu muhimu.

Akizungumza kwa niaba ya kocha mkuu wa Simba jana, kocha wa makipa, Mwarami Mohammed alisema kuwa wao wamejipanga vizuri kulingana na maandalizi waliyofanya hasa kambi ya Afrika Kusini pamoja na mechi za majaribio nchini humo.

Pia alisema hata mechi yao ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika ya raundi ya awali dhidi ya UD Songo ya Msumbiji, nayo imewasaidia kuwa fiti zaidi na kutamba kuwa wataifunga Azam leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Aliwataja wachezaji watakaowakosa mechi hiyo leo kuwa ni pamoja na Aishi Manula, Ibrahim Ajibu pamoja na Mbrazil Wilker da Silver, ambao wanasumbuliwa na maumivu. Mchezo huo wa ngao ya jamii unapigwa kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu mpya wa mwaka 2019/20, utakaoanza Agosti 23.

Mechi hiyo inawakutanisha Simba ambao ni mabingwa wa ngao hiyo na ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Azam FC ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho au FA, maarufu Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Simba msimu uliopita ilitwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Mtibwa Sugar kwa mabao 2-1 katika mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kwa upande wake, kocha msaidizi wa Azam, Iddi Cheche alisita kuweka wazi mipango ya kiufundi ya timu yao na kusisitiza kuwa hiyo ni siri ya benchi lao la ufuindi na kuahaidi kuleta upinzani na kutwaa ngao hiyo.

Alisema kupitia maandalizi waliyoyafanya kupitia michuano ya Kombe la Kagame na mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho na timu ya Ethiopia, wanaamini wamejiandaa vizuri kukabili Simba. Wenyewe Azam wamesema kuwa katika mchezo huo watawakosa wachezaji wao wawili, Bruce Kangwa na Mudathiry Yahya, ambao ni majeruhi.

Mudathir alipata maumivu katika timu ya taifa, Taifa Stars, katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) Misri wakati Kangwa aliumia katika mchezo uliopita wa Azam wa kimataifa Fasil Ketema ya Ethiopia. “Mchezo huu dhidi ya Simba hatuuchukulii poa, tumejipanga vizuri kama mechi zingine za kiushindani,“ alisema Cheche.

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi