loader
Picha

Mtifuano Ligi Kuu England kuendelea leo

LIGI Kuu ya England inaendelea tena leo kwa viwanja saba kutimua vumbi huku mabingwa watetezi Manchester City ni miongoni mwa timu hizo, yenyewe ikiangalia kulipa kisasi kwa Tottenham.

Man City, ambao wanaongoza ligi hiyo iliyoanza wiki iliyopita baada ya kushinda mchezo wake wa kwanza mabao 5-0 dhidi ya West Ham United, watataka kuendeleza makali katika mchezo huo wa leo.

Nao Tottenham Hotspurs baada ya mafanikio ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu uliopita, nao hawatakubali kufungwa kirahisi kwani katika Ligi Kuu ya England wamekuwa wakifanya vizuri katika misimu kadhaa licha ya kutotwaa taji.

Mabingwa wa Ulaya Liverpool na Manchester United nao pia watashuka kwenye viwanja tofauti wakiangalia kuendeleza makali yao baada ya kuanza ligi hiyo kwa ushindi. City ilikamilisha mataji matatu ya nyumbani msimu uliopita, lakini iliendelea kuvurunda katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya wakati Tottenham iliposonga mbele kutoka katika robo fainali kwa bao la ugenini.

Teknolojia ya VAR ilikataa bao lililofungwa na Raheem Sterling katika dakika za majeruhi katika mchezo wa marudiano wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya mabingwa wa Uingereza Aprili, huku Sterling akipiga hat-trick katika usiku huo na City ikitinga nusu fainali. Ndio, Sterling alianza kampeni upya, baada ya kupiga hat-trick katika ufunguzi wa ligi hiyo walipoifunga West Ham 5-0 na kushika usukani wa ligi hiyo.

Tottenham bayo iliifunga Aston Villa, lakini walihitaji kutoka nyuma na kufunga mabao mawili katika dakika tano za mwisho yaliyofungwa na Harry Kane na kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa iliyopanda daraja. Kane iliionya Spurs kuwa haitakiwi kuanguka mapema kama wanataka kushindania taji la msimu huu.

Liverpool wenyewe watakuwa wa kwanza kushuka dimbani siku hiyo kabla Man City na Spurs hawajakutana kwenye Uwanja wa Etihad, wenyewe wataifuata Southampton, ambayo katika mchezo wa kwanza ilifungwa 3-0 na Burnley katika mchezo wa kwanza wa msimu.

Mchezo mwingine wa leo Jumamosi utazikutanisha Arsenal ambayo itakuwa mwenyeji wa Burnley katika mchezo utakaoanza mapema saa 8:30 mchana, huku Aston Villa wenyewe wataikaribisha AFC Bournemouth na West Ham United wataifuata Brighton & Hove Albion.

Mechi zingine ni kati ya Norwich City, ambao wataikaribisha Newcastle United huku Everton wakikwaana na Watford katika mchezo mwingine wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 20.

Mchezo mwingine kesho utazikutanisha Sheffield United dhidi ya Crystal Palace utakaofanyika kwenye Uwanja wa Bramall Lane. Lampard arudi Nyumbani Chelsea ndio timu pekee ambayo kwa wale waliomaliza katika sita bora kuanza kwa kichapo katika ufunguzi wa Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa 4-0 na Manchester United katika mchezo wa kwanza Frank Lampard kuanza kuifundisha timu hiyo. Kiungo huyo wa zamani wa England akidai kuwa kipigo hicho kilikuwa kikubwa sana kwa timu yake baada ya kuanza vizuri mchezo huo.

Lakini Lampard baadaye alifarijika baada ya kikosi chake licha ya kufungwa kwa penalti katika Uefa Super Cup kwa Liverpool baada ya kutoka sare ya 2-2 katika mchezo uliofanyika Istanbul Jumatano.

Timu hiyo yenyewe itacheza mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu kesho Jumapili kwa kucheza dhidi ya Leicester City, wenyeji wakisaka kupata ushindi katika mchezo huo utakaofanyika mbele ya mashabiki wao kwenye Uwanja wa Stamford Bridge. Lampard ambaye ni mfungaji wa mabao mengi kwa wakati wote Chelsea, bado ana matumaini ya kupokewa vizuri katika uwanja huo wa nyumbani akitua mbele ya mashabiki wao kwa mara ya kwanza kesho.

QUIQUE Setien anasema kuwa hawezi kufi kiria jinsi alivyokuwa akiota ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi