loader
Picha

Rais Magufuli akabidhiwa uenyekiti SADC

RAIS John Magufuli amekabidhiwa rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) leo, Jumamosi, jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli anachukua madaraka hayo kutoka kwa Rais wa Namibia Dk Hage Geigob na ataongoza jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, jijini Dar es Salaam ambao umewaleta pamoja marais na viongozi wa serikali kutoka nchi 16 za jumuiya hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo Rais Magufuli amesema kuwa masuala ya viwanda yatapewa kipaumbele katika kipindi hiki cha uongozi wake.

“Tuna changamoto pia ya kutokuwa na mifumo mizuri ya uchumi wa viwanda, na hii ni sababu inayodumaza uchumi wetu kwenye jumuiya hii ya SADC,” ameongeza.

Hata hivyo Dk Magufuli ameitaka #Sadc kusimama pamoja na kuitetea Zimbabwe ili vikwazo vya kiuchumi dhidi yake viondolewe. Katika makabidhiano hayo, mwenyekiti anayemaliza muda wake ametumia fursa hiyo kutangaza Kiswahili kuwa lugha ya nne rasmi ya #Sadc.

Mbali na Kiswahili chenye mizizi yake, Tanzania, lugha nyingine rasmi katika mawasiliano ya #Sadc ni Kiingereza, Kireno na Kifaransa ambazo zinazungumzwa katika baadhi ya nchi wanachama.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi