loader
Picha

Mabalozi waombwa wawekezaji simu janja

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaomba mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania ughaibuni, kuwasaidia kutafuta wawekezaji watakaojenga kiwanda cha kutengeneza simu janja nchini.

Imesema simu zinazotumika nchini ni zaidi ya milioni 40 na kwamba kuna simu nyingi ambazo zimeisha matumizi yake na kutupwa hovyo, hivyo lazima kuwepo na kiwanda cha kuzikusanya.

Akizungumza katika ziara ya mabalozi 43 wa Tanzania wanaowakilisha nchi mbalimbali jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, James Kilaba alisema sekta ya mawasiliano ina fursa nyingi, lakini bado kuna changamoto.

Kilaba alisema changamoto kubwa ni namna ya upatikanaji wa simu janja kwa wananchi waliopo vijijini, hivyo uwepo wa kiwanda cha kuunganisha simu janja utasaidia kuunganisha maeneo yote nchini ikiwemo vijijini kwa kutumia mkongo wa taifa.

Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Naimi Aziz alisema wameona namna TCRA inavyoshirikiana na taasisi nyingine za mawasiliano kudhibiti mawasiliano na kuhakikisha kuwa Tanzania haiwezi kuathirika kwa njia yoyote kutoka nje.

Balozi Aziz alisema sekta hiyo imejipanga kwa kuwa na mitambo na wataalamu wa kudhibiti mawasiliano ili kuhakikisha masuala ya kiusalama yanawekewa mkazo kwa lengo la kulinda nchi dhidi ya mashambulizi yoyote ya kimtandao.

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi alisema wameona uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika kudhibiti mawasiliano ya kielektroniki na njia ya simu.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi