loader
Picha

Wakulima korosho wakopeshwa bil 1.3/-

WAKULIMA wadogo wa korosho 1,468 katika mikoa ya Lindi na Mtwara wamenufaika na mikopo ya Sh bilioni 1.3 kutoka Benki Yetu kwa mwaka 2018, imefahamika.

Hayo yalibainika jana katika taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki Yetu, Ernest Ndimbo katika mkutano Mkuu wa Nne wa Wanahisa wa benki hiyo uliofanyika, Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, Ndimbo alizitaja wilaya zilizonufaika katika mikoa hiyo kuwa ni Masasi, Liwale, Ruangwa, Lindi na Kilwa.

“Aidha, benki iliweza kutoa mafunzo kwa wakulima wadogo wa korosho juu ya matumizi tehama (teknolojia ya habari na mawasiliano) katikia kutumia huduma za benki kwa njia ya simu na matumizi ya ATM,” alisema.

Aliuambia mkutano huo kuwa, katika Mwaka wa Fedha wa 2018, Benki Yetu iliingia makubaliano na Shirika la Kimataifa la Misaada la USAID ya msaada wa kujengea uwezo wenye thamani ya Sh 333,498,282 na Water Org ya Marekani yenye thamani ya Sh 326,250,000.

“Misaada hiyo imetusaidia kuanzisha huduma maalumu kwa vijana katika kilimo chenye tija, kutoa huduma ya mikopo ya maji na maboresha mazingira…misaada hiyo ilitusaidia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi na vijana… Aidha, benki iliendelea kutoa mikopo ya kuboresha makazi vijijini katika Wilaya za Kilwa, Kibaha, Kilombero, Malinyi, Ulanga, Ruangwa na Masasi,”alisema.

Mkurugenzi wa Benki Yetu, Altemius Millinga alisema ili kuhakikisha ubora wa huduma, benki imeimarisha mifumo na matumizi ya tehama na kujitanua na kuwafikia wananchi wengi zaidi tena kwa ubora wa huduma.

Milinga alisema uzoefu wa benki hiyo unaonesha kuwa, bado elimu kuhusu hisa na uwekezaji inahitajika zaidi kwa Watanzania kwani wengi bado hawajui kutofautisha mikopo katika vikundi na uwekezaji kupitia umiliki wa hisa.

Mkurugenzi huyo wa Benki Yetu alisema, “wananchi wengi hasa wenye uwezo wananufaika sana na benki hii kupitia kujiajiri na kuendesha biashara kwani kwa kuwatambua hao, tunatumia dhamana mbadala, badala ya hati ya nyumba ambayo Watanzania wengi hawana.”

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi