loader
Picha

Tanzania yaongoza ukuaji uchumi SADC

KATIBU Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dk Stergomena Tax (pichani) amesema Tanzania ni nchi pekee katika jumuiya hiyo, iliyofanikiwa kufi kia kigezo kilichowekwa na jumuiya cha kufi kia ukuaji wa uchumi wa asilimia saba.

Dk Tax amesema SADC imejiwekea vigezo vya uchumi mpana wa kufikia asilimia saba na hadi sasa Tanzania ndio pekee iliyofika vigezo hivyo.

Stergomena ameipongeza nchi hiyo, kwa hatua hiyo ya mafanikio ;na kutaka nchi nyingine zipambane kufikia vigezo hivyo ili kwa pamoja kufikia malengo waliojiwekea.

Ameyasema hayo jana alipohutubia ufunguzi wa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC. Mkutano huo unawashirikisha viongozi wa nchi 16 za jumuiya hiyo. Dk Tax alisema ukuaji wa uchumi katika SADC, umeendelea kuimarika ingawa kuna changamoto nyingi.

Alisema mwaka 2017 ulikua kwa asilimia tatu na mwaka 2018 asilimia 3.1 huku nchi za Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Madagascar na Tanzania zikifanya vizuri.

Alisema Pato la Taifa katika kanda liliimarika kutoka Dola za Marekani 4,004 mwaka 2017 hadi Dola za Marekani 4,171 mwaka 2018.

Alisema mafanikio hayo, yamewezeshwa na nchi tano pekee ambazo ni Botswana, DRC, Maurituis, Shelisheli na Tanzania. Dk Tax pia alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi na kueleza jinsi SADC ilivyoshiriki katika majanga ya kimbunga Idai katika nchi za jumuiya hiyo.

Alimshukuru mwenyekiti aliyemaliza muda wake jana, Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob kwa juhudi kubwa za misaada ya kiutu zilizofanywa na nchi wanachama kwa nchi zilizopata matatizo hayo ya kimbunga Idai na Kenneth.

Alisema SADC ilitoa msaada wa Dola za Marekani 500,000 kwa nchi tatu zilizoathirika zaidi na kimbunga Idai na kufungua kampeni ya maafa iliyowezesha kukusanya zadi ya Dola za Marekani 203 kwa tatizo hilo.

Alisema eneo la kuwashirikisha vijana katika ubunifu na utatuzi wa ajira zilizoanzishwa na Dk Geingob zinaendelea kutekelezwa na sekretarieti ya SADC kwa kuhakikisha kunakuwa na fursa za ujasiriamali na biashara.

Alisema SADC inajivunia kuimarika kwa amani hasa katika nchi sita zilizofanya uchaguzi kipindi kifupi kilichopita katika jumuiya hizo ambazo ni eSwatini, DRC, Malawi, Zimbabwe, Madagascar na Comoro.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi