loader
Picha

Simba hii we acha tu

Tuzo Mapunda SIMBA imeanza vyema msimu huu baada ya kuifunga Azam mabao 4-2 katika mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.

Mechi hiyo inayoashiria kufungua pazia la Ligi Kuu Bara hushirikisha bingwa wa Ligi Kuu (Simba na bingwa wa Kombe la FA (Azam).

Simba sasa inatwaa ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo, msimu wa mwaka 2017/18 iliifunga Yanga, 2018/19 ikaifunga Mtibwa Sugar na jana msimu wa mwaka 2019/20 imeifunga Azam.

Azam ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 13 likifungwa na Shaaban Chilunda aliyewazidi kasi mabeki wa Simba na kuujaza mpira wa wavuni.

Dakika tatu baadaye, Sharaf Shiboub aliisawazishia Simba bao hilo akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Azam, Razak Abarola.

Shiboub alifunga bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jnr’.

Simba ilianza mashambulizi mapema mwa mchezo huo ikiliandama mara kwa mara lango la Azam kabla ya Wanalambalamba kukaa sawa na kurudisha mashambulizi.

Moto wa Simba uliendelea mpaka katika kipindi cha pili ambapo kama ilivyo kwenye kipindi cha kwanza walimiliki zaidi sehemu ya kiungo.

Dakika ya 57, Clatous Chama aliifungia Simba bao la tatu baada ya kuwatoka mabeki wa Azam na kuukokota mpira kabla ya kuachia shuti lililomzidi kipa Abalora. Dakika nne baadaye nusura Meddie Kagere aiandikie Simba bao lakini shuti lake lilipaa juu.

Mechi hiyo ilitawaliwa na ubabe na rafu nyingi, hali iliyomlazimu mwamuzi Elly Sasii kuwaonya kwa mdomo mara kwa mara hasa wachezaji wa Azam.

Hata hivyo, beki ya Simba ilikuwa ikikatika mara kwa mara na dakika ya 78 iliruhusu nyavu zake kutikiswa baada ya Azam kupata bao la pili lililofungwa na Frank Domayo akimalizia pasi ya Obrey Chirwa.

Francis Kahata alizidisha shangwe kwa Wanasimba baada ya kufunga bao la nne katika dakika ya 86 akiunganisha pasi ya Chama na kuachia mkwaju mkali kwenye lango la Azam.

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi