loader
Picha

Halmashauri zapewa mwongozo wa umwagiliaji

HALMASHAURI 22 za Kanda ya Dodoma ya Umwagiliaji zimepewa mwongozo wa kitaifa wa umwagiliaji utakaosaidia kuinua sekta ya uwagiliaji katika maeneo hayo.

Mwongozo huo umeandaliwa chini ya utekelezaji wa Mradi wa kujengea uwezo wataalamu wa kilimo na wakulima wadogowadogo Awamu ya Pili (TANCAID II) unaotekelezwa katika halmashauri 61 chini ya Ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA).

Akizungumza kabla ya kukabidhi mwongozo huo, Mhandisi wa Tume ya Uwagiliaji ambaye ni mratibu mwenza wa utunzaji na ukarabati wa skimu, Amy Mchelle alisema hatua hiyo inatoa fursa kwa maofisa kilimo, umwagiliaji na ushirika na wakurugenzi kutumia mwongozo huo katika kuibua miradi ya umwagiliaji, ujenzi wa miradi hiyo na utunzaji na uendeshaji wake.

“Mradi wa TANCAID umetekelezwa katika halmashauri 61 nchini, lakini halmashauri 36 ndizo zilizopewa msukumo mkubwa.

Halmashauri 22 za Kanda ya Dodoma tunazikabidhi mwongozo wa taifa wa umwajiliaji ili wakautumie katika kuibua miradi, kutekeleza, kutunza na kuiendesha miradi ya umwagiliaji katika maeneo yao,”amesema.

Kanda ya Dodoma ya Umwagiliaji inahusisha halmashauri za wilaya ya mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Manyara. Aidha, Mchelle alizitaka halmashauri husika kuhakikisha zinatenga fedha kwenye bajeti zao ambazo zitatumika kutunza na kukarabati miundombinu ya skimu za umwajiliaji katika maeneo yao.

Kaimu Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika kutoka Wilaya ya Simanjiro, Fabian Malabila amesema miongozo hiyo itawasaidia katika kuimarisha sekta ya umwagiliaji kwa kuibua miradi, kujenga na namna bora ya kuiendesha na kuitunza.

Amesema kupitia wa mradi wa TANCAID II kwa wilaya yake ulihusisha skimu tatu za umwagiliaji ambazo ni Lemkuna, Ngage na Kambi ya Chokaa ambayo kwa sasa imekuwa ikifanya vizuri katika kilimo cha umwagiliaji.

“Mradi wa TANCAID II umetusaidia sana kwani skimu hizi tatu miundombinu yake kwa sasa imekuwa mizuri, hata uzalishaji umeongezeka maradufu, kwa mfano Skimu ya Lemkuna awali mavuno ya mpunga yalikuwa kati ya tani tano hadi sita kwa hekta, lakini sasa ni zaidi ya hekta tisa…,” amesema.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi