loader
Picha

Magufuli- Kiswahili SADC heshima kwa Nyerere

Mwenyekiti wa Jumuiya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Rais John Magufuli amesema, uamuzi wa wakuu wa nchi na viongozi wa jumuiya hiyo kukubali lugha ya Kiswahili iwe lugha rasmi SADC ni heshima kubwa kwa Baba wa Taifa la Tanzania Julius Nyerere.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati anafunga Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na viongozi wa SADC.

Amesema, uamuzi huo ni wa kihistoria na umefuta machozi ya Baba wa Taifa.

"Lugha ni chombo muhimu katika kuimarisha mahusiano baina ya watu lakini pia katika kukuza na kuimarisha ushirikiano na utengamano kati ya mataifa" amesema.

Rais Magufuli amesema Kiswahili ni lugha ya kiafrika na wao (wanachama SADC) ni Waafrika hivyo ana imani uamuzi huo utasaidia kuimarisha uhusiano wa wananchi kwenye jumuiya hiyo, kukuza na kuimarisha ushirikiano mtengamano kati ya nchi wananchama.

"Na nitumie fursa hii kusihi nchi wanachama ambako Kiswahili hakitumiki kuiga mfano wa Afrika Kusini ambapo kuanzia mwakani itaanza kufundisha kwenye shule zake. Sisi Tanzania tutakuwa tayari kuwaunga mkono ikiwemo kwa kutoa walimu na nyenzo mbalimbali za kufundishia" amesema Magufuli.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa SADC, jana aliwapa marais wenzake vitabu vya Kiswahili waende navyo kwao, na wamevipokea vizuri.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi