loader
Picha

Tanzania ilipambana kuikomboa Zimbabwe

ZIMBABWE ni moja ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) isiyo na bahari. Nchi hii inayoongozwa na Rais Emmerson Mnangagwa.

Ni miongoni mwa nchi ambazo Tanzania ilisimama kidete kuhakikisha zinapata uhuru. Tanzania ilikuwa na jukumu muhimu katika mataifa ya kusini mwa Afrika, kuhakikisha yanakombolewa kutoka katika utawala wa wakoloni.

Mnangagwa alikuwa miongoni mwa wapigania uhuru kutoka nchi za kusini mwa Afrika, waliopewa hifadhi nchini wakati wa harakati hizo.

Chuo cha Kilimo cha Kaole kilichopo Bagamoyo ni miongoni mwa maeneo yaliyohifadhi historia hiyo, kwa kuhifadhi wapigania uhuru hao akiwamo Mnangagwa.

Alipotembelea nchini mwaka jana, Rais Mnangagwa alitembelea chuo hicho. Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo hicho cha Kaole kinachoendeshwa na Jumuiya ya Wazazi, Sinani Simba, historia yake inaanzia mwaka 1963 pale Rais wa Tanzania wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere alipotoa eneo hilo kwa chama cha Frelimo cha Msumbiji kuhakikisha Afrika yote inakuwa huru.

“Wakati ule ukombozi ulikuwa ushirikiano wa nchi mbalimbali. Hapa waliokuwapo wapigania uhuru kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe na Rais wa sasa wa Zimbabwe, Mnagangwa alikuwapo,” anasema Simba.

Wapigania uhuru hao walitumia kambi hiyo, kujifunza mbinu mbalimbali za kupigania nchi zao. Pia kulikuwa na chuo cha ufundi hususani useremala na umakenika. Kutokana na ushirikiano wa nchi hizo za kusini mwa Afrika, Zimbabwe ambayo ilijulikana kama Southern Rhodesia, ilipata uhuru wake Aprili 18, 1980.

“Upo umuhimu mkubwa wa kuelimisha kizazi cha sasa juu ya harakati za ukombozi…Mimi naelewa mchango wa Tanzania katika kupigania uhuru wetu lakini kipo kizazi kipya kisichofahamu au kuthamini. Waelimishwe,” anasema Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Samuneti Leathers, Clive Chirova.

Chirova ambaye alishiriki maonesho ya nne ya viwanda ya SADC jijini Dar es Salaam, anasema mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, yamechangia kizazi cha sasa kutothamini historia ya ukombozi wa nchi za Afrika.

Mshiriki mwingine wa maonesho kutoka Zimbabwe, Rosemary Vambe anasema, “Tanzania ni mama na baba wa nchi nyingi za Kusini mwa Afrika. Licha ya msaada wa kisiasa iliotoa wakati wa ukombozi, mpaka sasa ni kitovu cha biashara kwa nchi nyingi hususani zisizo na bahari kutokana na kutumia bandari ya Dar es Salaam”.

Zimbabwe yenye eneo la kilometa za mraba 390,757, inapakana na Msumbiji (Mashariki), Zambia (Kaskazini na Kaskazini Magharibi), Afrika Kusini (Kusini) na Kusini Magharibi inapakana na Botswana.

Ina idadi ya watu 12,754,000 na lugha rasmi ni Kiingereza na Kishona na Kindebele, zinazozungumzwa sehemu kubwa ya nchi. Mji mkuu wa Zimbabwe ni Harare, ukisifika kuwa wa kibiashara na kituo cha viwanda. Miji mingine ni Bulawayo na Mutare.

Tegemeo kubwa la uchumi wa Zimbabwe ni mazao ya kilimo hususani tumbaku, pamba na miwa. Mazao yanayosafirishwa kwa wingi nje ya nchi ni tumbaku na maua.

Mazao mengine ambayo husafirishwa (si kwa kiwango kikubwa) ni sukari, majani ya chai, kahawa, pamba, mbegu na nafaka. Soko la nje la mazao ya kilimo liko Marekani, Ulaya, Afrika na Mashariki ya Mbali.

Madini huchangia asilimia 4.3 ya pato la ndani (GDP) na huchangia asilimia saba ya ajira nchini . Pia huchangia asilimia 40 ya fedha za kigeni.

Zimbabwe inatajwa kuwa nchi iliyobarikiwa kwa utajiri wa madini kutokana na kuwa na zaidi ya aina 40 ikiwamo dhahabu, makaa ya mawe, bati, shaba, almasi.

Utalii huchangia asilimia tano ya GDP na ajira 83,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Utalii wa wanyama na maeneo ya asili ndiyo unaotawala sekta hiyo. Vivutio vingine vya utalii nchini humo ni maporomoko ya Victoria, makazi ya watawala wa zamani na Ziwa Kariba.

Kwa kipindi kirefu kumekuwa na mikakati ya kuongeza pato la ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi