loader
Picha

Chuo cha Nyerere 'kupika' viongozi

VIONGOZI wa vyama vya siasa vilivyosaidia ukombozi katika nchi zilizopo kusini mwa Bara la Afrika wametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo Cha Uongozi Cha Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani.

Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Dk Bashiru Ally viongozi hao wamefika katika eneo hilo na kushuhudia ujenzi ukiendelea kwa kasi chini kampuni ya ujenzi ya CRCJE kutoka nchini China.

Ujenzi wa chuo hicho unahusisha ushirikiano wa vyama sita vya ukombozi barani Afrika ambavyo ni CCM (Tanzania) FRELIMO (Msumbiji), ANC (Afrika Kusini), SWAPO (Namibia), ZANU-PF na MPLA (Zimbabwe).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally amesema sababu kuu ya ziara hiyo ni kuwawezesha viongozi hao kuona maendeleo ya ujenzi unaotarajiwa kukamilika kati ya Juni au Julai mwakani.

Amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutawezesha kusaidia 'kuwapika' na kuwakumbusha vijana misingi ya uongozi bora iliyoasisiwa na waasisi wa ukombozi wa mataifa hayo ili waweze kuiga na kuzisaidia nchi zao katika maendeleo.

“Tunaamini pindi chuo hiki kitakapokamilika kitaweza kutoa mafunzo mbalimbali ya uongozi yatakayoweza kuwapika vijana kiuongozi na kuwawezesha kuwa viongozi bora katika Bara hili kupitia nchi zao,” amesema Dk Bashiru.

Chuo hicho kitakuwa na uwezo wa kutoa mafunzo ya muda wa miezi mitatu, mafunzo ya kati ya mwaka mmoja, na mafunzo ya muda mrefu ya miaka mitatu.

Dk Bashiru amesema, ujenzi wa chuo hicho ni muhimu kwa kuwa kitatumika kuwapa vijana mbinu za uongozi kuwawezesha kuwa na weledi wa kutosha kiuongozi na hivyo kuwa chachu ya maendeleo na kutetea maslahi ya nchi zao.

Aidha ujenzi wa Chuo hicho ni muendelezo wa CCM kuweka mkazo katika mafunzo ya viongozi na makada wake na kwa sasa kuna ujenzi wa vyuo vingine vidogo vya Ihemi- Iringa, Tunguu- Zanzibar, Katunguru- Mwanza na Kaole- Pwani

Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed (CUF) amejiuzulu kiti ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi