loader
Picha

Kiswahili SADC fursa kwa Watanzania

BAADA ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC), kupitisha Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne Sadc, wasomi wamesema lugha hiyo itachochea masuala mengi na Watanzania wajipange kutumia nafasi hiyo kufundisha huko.

Wasomi hao wamesema uamuzi wa lugha ya Kiswahili kutumika katika Sadc ulisubiriwa kwa muda mrefu na sasa yametimia.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa SADC, Dk Hage Geingob akihutubia mkutano huo juzi jijini Dar es Salaam katika vikao vilivyomalizika jana, alitangaza Kiswahili kitakuwa lugha ya nne sambamba na Kingereza, Kifaransa na Kireno.

Mtaalamu wa Kiswahili Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Oni Sigala alisema nafasi ya Kiswahili kutumiwa na nchi za Afrika ilisubiriwa kwa muda mrefu ambapo aliwaasa Watanzania kujipanga kutumia fursa hiyo.

“Hili ni jambo jema na tulilitegemea miaka mingi lakini sasa imefikia,” alisema Sigala.

Alisem hiyo ni fursa nzuri Watanzania kwenda kufundisha lugha hiyo katika nchi hizo na wasisubiri serikali bali waende mmoja mmoja.

Alisema wataalamu wa lugha hiyo ambayo ndio lugha kuu nchini wapo wengi ambao anaamini ndio watu sahihi kwenda kufundisha lugha hiyo kwa ufasaha kuliko watu wa nchi nyingine.

Mhadhiri na Mchambuzi wa Masuala ya Kidiplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam, Israel Sosthenes alisema huu ni wakati sahihi kwa lugha ya Kiswahili kutumiwa katika nchi hizo ikizingatiwa ilitumiwa na wapigania Uhuru katika nchi nyingi za Afrika.

Mhadhiri huyo alisema pia kuwa mbali na jambo hilo, lugha hiyo itachochea masuala ya kiuchumi na kijamii katika nchi za Afrika.

“Kiswahili ni lugha ya ukombozi, ilitumiwa na wapigania Uhuru katika ukombozi wao hivyo ni sahihi kuanza kutumika katika nchi za Sadc na nchi hizo kwa ujumla,” amesema Sosthenes.

Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa aliwapongeza wakuu wa nchi kwa kuingiza lugha hiyo kuwa rasmi kwa ukanda huo ambapo aliwataka watanzania kujipanga kwa fursa hiyo.

Amesema Kiswahili ni fahari, inazidi kuingia katika vyombo vya kimataifa ambapo alisema kuwa ana imani kuwa lugha hiyo itazidi kukua.

Awali Rais John Magufuli alisema Kiswahili ni lugha ya 10 duniani kuzungumzwa na watu wengi, ya 13 Afrika na ya sita katika Sadc.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), inatarajia kulipeleka kwa ...

foto
Mwandishi: Regina Mpogolo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi