loader
Picha

Asasi yasaidia majeruhi wa moto, vifo zaidi vyaripotiwa Muhimbili

TAASISI ya Lions Club imetoa msaaada wa vitu kwa majeruhi wa moto wa Morogoro, wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Misaada iliyotolewa na taasisi hiyo mwishoni mwa wiki ni pamoja na 'pampers' na sindano kwa ajili ya waathirika wa moto ambao hadi Jumapili, jumla ya vifo 95 vilikuwa vimekwisharipotiwa.

Akizungumza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam, kiongozi wa Lions Club, Shabbir-hussein Khalfani alisema: "tumeguswa na tukio la janga la moto lililowapata wenzetu. Tukiwa sehemu ya jamii tumewasilisha msaada wetu wa vitu mbali mbali vyenye thamani ya shilingi milioni mbili."

Aliongeza kuwa kuna mahitaji mengine ambayo MNH wamehitaji kwa ajili ya wagonjwa hao ikiwemo gozi za kusafishia vidonda na kuahidi kuwa misaada hiyo itawasilishwa hospitalini hapo mapema ili iweze kusaidia wagonjwa.

Naye Mkuu wa idara ya utasishaji hospital ya Muhimbili, Batusaje Mwaibanje alitoa shukrani zake za dhati kwa taasisi hiyo huku akisisitiza kuwa msaada uliotolewa ni muhimu hasa kipindi hiki ambacho kuna wagonjwa wa dharura wa ajali ya moto.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini, Rajabu Mtiula ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro, Dar es Salaam

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi