loader
Picha

Magufuli aanza kwa kasi SADC

NCHI wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), zimeguswa na kasi ya uongozi wa Rais John Magufuli kutokana na alivyoendesha mkutano wa wakuu wa nchi na serikali kwa ufanisi kipindi kifupi, baada ya kukabidhiwa uenyekiti.

Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi, ameeleza kuguswa na uongozi wa Magufuli wakati akitoa neno kwa niaba ya wakuu wa nchi na serikali za SADC kwenye mkutano wao wa 39 uliohitimishwa jana jijini Dar es Salaam.

“Nataka kukupongeza kwa jinsi ulivyoongoza mkutano huu,...umezaliwa jana tu (kwa maana ya kukabidhiwa uenyekiti wa SADC) lakini umekuwa mtoto mkali wa kukimbia kabisa,” alisema na kushangiliwa ukumbini.

Amemtakia Rais Magufuli majukumu mema ya uenyekiti na kuahidi kuwa nchi wanachama, zitashirikiana naye bega kwa bega.

“Usiwe na wasiwasi sisi tutakufuata,” alisema Nyusi ambaye nchi yake inatarajiwa mwakani kupokea kijiti cha uenyekiti kutoka kwa Rais Magufuli na kuongoza mkutano wa 40 wa jumuiya hiyo.

Rais huyo wa Msumbiji, alipongeza mapokezi waliyopata nchini na namna Rais Magufuli alivyoshirikiana naye wakati nchi yake ilipokumbwa na kimbunga kilichosababisha vifo vya watu wengi na uharibifu wa mali.

“Magufuli alinipigia simu kuomba nimtaarifu hali ilivyo ili aweze kusaidia. Tunashukuru sana kwa msaada mliotupa na kututia moyo,” alisema Rais Nyusi, ambaye pia alizishukuru nchi wanachama wa SADC zilivyoshirikiana nao katika janga hilo.

Aidha, aliwaambia wakuu wa nchi na serikali kuwa watakapokwenda Msumbiji mwakani, atawakaribisha kwa mikono miwili.

“Nawakaribisha katika mkutano wa 40 utakaofanyika Maputo,” amesema.

Wakati huo huo, Rais Nyusi alimpongeza mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda wake, Rais wa Namibia, Dk Hage Geingob kwa kuwa kiongozi aliyeonesha mfano kwa jumuiya.

Juzi baada ya kukabidhiwa uenyekiti, Rais Magufuli katika hotuba yake aliweka wazi msimamo wa mambo anayotaka yafanyike, kwa kusisitiza kuwa nchi za Kusini mwa Afrika si masikini, bali zinatakiwa zihakikishe zinatumia vyema raslimali zake kuwanufaisha wananchi.

Alisema anajua kazi ya uenyekiti wa SADC si rahisi ; na kuanisha matatizo yanayokabili ukanda huo, ikiwemo uchumi kutokua na kuinyooshea kidole Sekretarieti ya SADC na kutaka ifanye kazi kwa ufanisi kuhakikisha matatizo hayo yanapatiwa suluhu.

Msimamo mwingine alioweka wazi kupitia mkutano huo ni kuhusu vipaumbele vyake, kwa kusisitiza kwamba katika kipindi cha uenyekiti wake, maendeleo ya viwanda yatakuwa kipaumbele chake na akataka kila nchi kuzingatia hilo.

Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed (CUF) amejiuzulu kiti ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi