loader
Picha

Hongera Watanzania kufanikisha SADC

MKUTANO wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ulimalizika jana jijini Dar es Salaam kwa viongozi wakuu wa nchi wanachama, kutoa tamko la makubaliano ya mpango kazi wa kutekeleza maazimio mbalimbali waliyofi kia juzi.

Kufuatia kumalizika kwa mkutano huo, viongozi wakuu wa nchi wanachama walianza kuondoka kurudi kwao, wakiacha jukumu la usimamiaji maazimio hayo kwa Tanzania, ambayo Rais Dk.John Magufuli alipokea kijiti cha uenyekiti wa SADC juzi pia.

Mkutano huo umemalizika kwa amani na utulivu mkubwa, ukiacha historia ya aina yake kwa wananchi wa Tanzania na wageni walioshiriki mkutano huo tangu uanze wiki mbili zilizopita, kwa maonesho ya wiki ya viwanda SADC na mikutano ya mawaziri wa Sadc.

Tunapenda kuungana na Watanzania wote na pia Rais Magufuli kuwashukuru wageni wote, viongozi wa nchi wanachama wa SADC, mawaziri wao, makatibu wakuu na maofisa wengine waandamizi na wasaidizi wao na wageni, waalikwa kwa ushiriki wao.

Ushiriki wao ulikuwa muhimu katika kufanikisha mkutano huo wa kikanda, kwa kuzingatia kuwa umefanyika katika nchi ambayo ilikuwa mwenyeji wa viongozi wa nchi hizo wakati wakipigania uhuru wa nchi zao na hivyo uliwarejesha katika historia hiyo.

Ni kwa msingi huo, tunasema kama nchi tulifurahia uwepo wao, ushiriki wao katika mkutano na michango mbalimbali waliyotoa kwa ajili ya kujenga misingi ya uhusiano wa kidiplomasia, uchumi na jamii ya watu wao kwa lengo la kuwaletea maendeleo zaidi.

Tunatoa pongezi nyingi kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa kufanikiwa kusimamia na kudhibiti amani na usalama kwa muda wote wa mkutano huo tangu kuwasili, kuishi na kuondoka kwa wageni hao na baada ya hapo bila matatizo yoyote.

Kufana kwa mkutano huo, kumezidi kudhihirisha nguvu ya Tanzania katika medani ya siasa za kimataifa katika masuala ya amani na usalama, ustawi wa demokrasia na uchumi.

Hali hiyo ilimfanya Rais wa Namibia, Hage Geingob kueleza kuwa Tanzania ni nchi ya mfano, hasa jinsi inavyoenzi viongozi wakuu wastaafu.

Ni matarajio yetu kuwa wageni hao wakiongozwa na viongozi wao wakuu, watakuwa wamefurahia ukarimu walioonyeshwa na watafikisha salamu zetu kwa ndugu zao na wananchi wao. Kwao wote, tunasema Asanteni sana kwa kuja na karibuni tena!.

TAHADHARI iliyotolewa juzi na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi