loader
Picha

Simba- Songo waje tupo tayari

Kocha wa Simba Patrick Aussems amesema ushindi dhidi ya Azam kwenye mechi ya Ngao ya Jamii umekiimarisha zaidi kikosi chake kuelekea mechi dhidi ya UD Songo ya Msumbiji.

Simba inatarajiwa kucheza mechi ya marudiano ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii, mechi ambayo Simba inahitaji ushindi wowote baada ya kutoka suluhu ugenini wiki mbili zilizopita.

Timu hiyo juzi ilitwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Azam mabao 4-2 katika mechi iliyokuwa ya vuta nikuvute huku wachezaji wa pande zote wakishambuliana kwa zamu.

Akizungumza baada ya mechi hiyo juzi, Aussems alisema amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake na hiyo ni taa ya kuwakabili wapinzani wao kwenye michuano ya kimataifa.

Matokeo hayo ya ushindi yamewafanya Simba kuchukua ngao hiyo kwa mara ya tano wakifikia rekodi iliyokuwa inashikiliwa na watani wao Yanga.

Huku Mabingwa hao wa Ligi Kuu wakitwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

Aussems alisema wachezaji wake kila siku zinavyokwenda wanaonesha ubora ambao anatamani kuuona kuelekea kwenye mechi dhidi ya UD Songo.

“Kiukweli nimeridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji kulingana na ushindi tuliopata leo (juzi) bado unazidi kutupa morali kule tunaokoenda…

“Sasa baada ya mechi hiyo tunajipanga na mechi dhidi ya wapinzani wetu, tunataka kupata matokeo mazuri kwasababu lengo ni kufika mbali zaidi kwenye michuano hiyo msimu huu kuliko ilivyokuwa msimu uliopita,” alisema.

Msimu uliopita Simba iliishia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. “Lakini kikubwa ushindi wa leo (juzi) ni zawadi tosha kwa mashabiki wa timu yetu kuwakaribisha kwenye ufunguzi wa msimu mpya wa ligi,”alisema Aussems.

Aidha alisema, hawezi kubweteka na ushindi wa Azam ambayo anasema kwake ni miongoni mwa timu zenye ushindani mkubwa lakini kama Simba maandalizi yao yamejikita kwenye kuhakikisha wanatimiza malengo waliyojiwekea kwa msimu huu.

Akizungumzia wachezaji wake majeruhi, Aussems alisema wachezaji hao ambao ni Ibrahimu Ajibu, Aishi Manula na Willker Dar Silver wanaendelea vyema na kwamba muda sio mrefu watakuwa fiti kujiunga na kikosi.

Kwa upande wake kocha msaidizi wa Azam Iddi Cheche alisema wamekubali matokeo na kwamba mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi hiyo wanaenda kuyafanyia kazi kujipanga na michezo inayokuja.

“Siku zote mpira ni mchezo wa makosa tulitengeneza nafasi nyingi tumetumia chache wenzetu wamefanya vizuri tunaenda kujipanga

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi