loader
Picha

Tshishimbi arudisha kicheko Yanga

PAPY Tshishimbi jana aliifungia Yanga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi ya kirafi ki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya uliochezwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Iliilazimu Yanga kusubiri mpaka dakika ya 83 kuandika bao hilo katika mechi hiyo iliyokuwa ya vuta nikuvute.

Tshishimbi alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Patrick Sibomana.

Kabla ya bao hilo, Tshishimbi alikosa bao la wazi katika dakika ya 13 baada ya kupiga kichwa kilichokwenda pembeni ya lango akibaki peke yake na kipa wa Leopards.

Hiyo ni mechi ya pili Kanda ya Kaskazini kwa Yanga baada ya kufungwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania Ijumaa kwenye uwanja wa Ushirika Moshi.

Kocha Mwinyi Zahera ametumia vikosi viwili tofauti katika mechi hizo akisisitiza kutaka wachezaji wanaotambua sababu ya kusajili na timu hiyo.

Timu hiyo inajiandaa na mechi ya marudiano ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers ya Botswana itakayofanyika mjini Gaborone mwishoni mwa wiki hii.

Yanga inahitaji ushindi katika mechi hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na ...

foto
Mwandishi: Yasinta Amos, Arusha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi