loader
Picha

Jokate- Yanga bingwa msimu huu

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Joketi Mwegelo, ameitabiria Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Joketi alisema alipojumuika na wanayanga wenzake kwenye uzinduzi wa tawi la Yanga Kisarawe mjini, alieleza Yanga ni timu ya wananchi na wawekezaji ni wananchi hivyo wanakila sababu ya kutembea kifua mbele kuhakikisha wanatwaa ubingwa msimu huu.

“Sisi ni Yanga na Yanga ni ya wananchi, tunakila sababu ya kutwaa ubingwa msimu huu hivyo wanayanga wanatakiwa watembee kifua mbele kuhakikisha wanaendeleza historia yao ya kuwa mabingwa wa kihistoria msimu huu,” alisema.

Aidha, alisema amefanya uzinduzi wa tawi hilo kama moja ya tawi lake la nyumbani kipindi hiki ili kuongeza chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu kwa wilaya ya Kisarawe.

Mwenyekiti wa tawi hilo, Mohamed Maurus, alisema tawi hilo lenye wanachama 150 ni moja ya matawi mama wilaya ya Kisarawe katika kuinua na kuendeleza timu yao kuhakikisha wanaiunga mkono timu yao kwa hali na mali msimu huu.

Alisema wanayanga wa Kisarawe wametoa nishani maalumu ya uvumilivu kwa kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, kutokana na hali ya ukata aliyopitia msimu uliopita lakini aliiongoza timu hiyo kumaliza ya pili kwenye Ligi Kuu.

Uzinduzi huo ulipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa Kisarawe na nje ya Kisarawe.

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na ...

foto
Mwandishi: Mohamed Masenga, Pwani

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi