loader
Picha

Madiwani CCM wapinga kununuliwa Ipad

MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali kuingilia kati na kuzuia matumizi ya zaidi ya Sh milioni 104 zinazotarajiwa kununua Ipad za madiwani.

Wameomba fedha hizo zisinunue Ipad kama ilivyopangwa na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala yake zitumike kukarabati miundombinu ya barabara kwenye vijiji na kata za halmashauri hiyo.

Diwani wa Kata ya Okaoni, Moris Makoyi (CCM), alisema fedha hizo zilipangwa zitumike kukarabati barabara baada ya kipindi cha mvua za masika kumalizika, lakini madiwani wa Chadema na Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila, wameamua zitumike kununua Ipad za madiwani na baadhi ya wataalam.

“Hii ni rushwa kwa sababu wanakaribia kumaliza muda wao, vyoo vya wanafunzi mashuleni vimeanguka, zahanati hazina umeme, wakinamama wanashindwa kwenda kujifungua na wagonjwa wanafariki njiani kwa sababu barabara ni mbovu halafu wanataka kununua Ipad,” alisema.

Alisema kipaumbele ni wananchi kupata maendeleo badala ya viongozi kujinufaisha wenyewe kwa vitu ambavyo havina msingi na kudai kuwa, mwenyekiti wa halmashauri hiyo amekuwa akipeleka miradi mingi ya maendeleo kwenye kata za Chadema.

Diwani wa Kata ya Kahe Mashariki, Kamili Mmbando (CCM), aliomba serikali izuie matumizi ya fedha hizo akisema ni ufisadi ndani ya halmashauri kwani zikinunuliwa Ipad zitatumika zaidi kwa matumizi binafsi.

Diwani wa Kilema Kaskazini, Anna Lyimo (CCM), aliwataka madiwani wakumbuke kuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi hivyo hawatakiwi kutumia vibaya fedha za umma bali zitumike kuleta maendeleo kwenye kata.

Akijibu hoja za madiwani hao wa CCM, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi, Kilawila alisema halmashauri hiyo inaendeshwa bila kuangalia itikadi za vyama na kwamba waliamua kununua Ipad kwa ajili ya kupunguza matumizi ya kutoa nakala kivuli na usafiri wa kusambaza nyaraka za madiwani kwenye kata 32.

“Tuliamua kuingia kwenye mfumo wa dijitali kwa sababu madiwani na wataalam wakiwa na Ipad itapunguza gharama za kutumia makaratasi na kutoa nakala kivuli na hatuna sababu za kupinga kwa sababu halmashauri nyingine zimefanya hivyo,” alisema.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Flora Mwakasala, Moshi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi