loader
Picha

Mkutano SADC wainufaisha ATCL

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) ni moja ya sekta zilizonufaika na Mkutano wa 39 wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana jijini Dar es Salaam.

Aidha, shirika hilo limeazimia kumaliza changamoto za ucheleweshaji wa safari, uahirishaji wa safari na utoaji wa taarifa kwa abiria pindi kunapokuwa na hitilafu ili kuondoa adha hiyo kwa abiria na kuwapo sokoni kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungwa kwa mkutano wa nne wa Baraza la Wafanyakazi la ATCL jijini Dar es Salaam.

Kuhusu mkutano wa SADC, mkurugenzi huyo wa ATCL alisema shirika hilo limenufaika kwa kuwa kati ya marais 15 waliofika nchini kuhudhuria mkutano huo, Rais wa Comoro alitumia ndege ya shirika hilo kwa safari ya kuja na kurudi nchini kwake.

Alisema wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano huo pia wametumia usafiri wa shirika hilo kuja nchini na kurudi katika nchi zao.

Kuhusu changamoto zinazolikabili shirika hilo, Matindi alisema linaingia katika soko la kimataifa ikiwa tayari limepata ufumbuzi changamoto mbalimbali ikiwamo ya ucheleweshaji wa ndege kwa abiria.

“Kwa mfano suala la ucheleweshaji wa ndege hakuna anayetaka ila sababu zinazotokana na uzembe zikomeshwe na zile nyingine kuwe na mpango wa kudhibiti hali hiyo mapema.”

“Ucheleweshaji mara nyingine unatokana na kuharibika kwa ndege na kwa kuwa ni chache zinafanyika jitihada za kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa,” alisema.

Kwa upande mwingine, Matindi alisema kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi sita wamekuwa wakipata soko la mizigo kwani wamesafirisha tani 59 za mizigo kutoka India kuja Tanzania.

“Mizigo hiyo ikifika Tanzania ipo inayobaki hapa hapa na mingine inapelekwa nchi nyingine,” alisema.

Alisema wanaendelea na mazungumzo na nchi za Botswana na Namibia ili wanapopeleka abiria Afrika Kusini wawe wanachukuliwa kutoka hapo na kupelekwa katika nchi hizo.

Akifunga baraza hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ATCL, Emmanuel Koroso, alisema bodi hiyo mpya ina mtazamo mpya tofauti na ya zamani ambayo ilikuwa na mikataba isiyoeleweka pamoja na watu kuweka maslahi binafsi hali iliyozorotesha shirika hilo.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi