loader
Picha

Naibu Katibu Mkuu viwanda aapishwa

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, amemuapisha Khadija Khamis Rajab kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda.

Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Said Hassan Said na Naibu Waziri Wizara ya Biashara na Viwanda, Hassan Khamis Hafidh.

Wengine waliohudhuria ni Naibu Kadhi Mkuu, Sheikh Othman Ngwali, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahamoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Khatib Abrahman Khatib, washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa serikali pamoja na wana familia.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Khadija alimshukuru Rais Dk Shein kwa kumuamini na kumkabidhi wadhifa huo kwa maslahi ya taifa. Aliahidi kufanya kazi zake kwa juhudi na maarifa na kufuata miongozo na sheria zilizopo ili kuharakisha kasi ya kuliletea taifa maendeleo.

Aidha, aliahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wafanyakazi wa wizara hiyo pamoja na viongozi wa serikali ili kuleta ufanisi.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi