loader
Picha

TRA yakana kutangaza ajira 500

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekanusha habari inayosambaa katika mitandao ya kijamii, ikidai kuwa TRA kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imetangaza nafasi za kazi 500 za uelimishaji uchangiaji kodi na ukusanyaji wa kodi ya majengo vijijini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi ya TRA, wananchi wameombwa kuipuuza habari hiyo.

“TRA inakanusha taarifa hiyo na inauomba umma kuipuuza kwa sababu haina ukweli wowote,” ilifafanua taarifa hiyo ya TRA jana.

Taarifa hiyo imesema hata mawasiliano ya kwenye habari hiyo si rasmi ya TRA hivyo wananchi wawe makini ili kuepuka kutapeliwa.

Kumekuwepo na taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari, “Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha pamoja na Benki Kuu (BOT)” kutangaza ajira 500.

Hatua hiyo ndiyo iliyoifanya TRA kukanusha na kutahadharisha wananchi kuhusu taarifa hiyo. TRA imewaomba wananchi kupiga simu bure Kituo cha Huduma kwa Wateja kupitia namba 0800 750 075 au 0800 780 078 au kutuma barua pepe: huduma@tra.go.tz, au kutembelea tovuti www. tra.go.tz.

Pia, wanaweza kutuma ujumbe kwa njia ya WhatsApp kwenda namba 0744-233-333 ili kupata ufafanuzi wa masuala yao.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi