loader
Picha

Ndugu 3 mbaroni tuhuma za mauaji

JESHI la Polisi mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wanne, kati yao watatu wa familia moja wakidaiwa kuhusika na mauaji ya mtoto wa shangazi yao, Kalekwa Shiku (50) kwa kumpiga kichwani na usoni kwa kitu chenye ncha kali.

Watu hao wanne wanadaiwa kumuua mtoto wa shangazi yao huyo, Kuyonza Kubeja (30) wakiwa na lengo ovu la kupora mali zake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Richard Abwao akizungumza na waandishi wa habari amethibitisha kutokea mauaji hayo.

Amesema mauaji yalitokea Juni 18, mwaka huu katika kitongoji cha Mwakundi, kijiji cha Mishepo, kata ya Mwantini ambapo Kalekwa aligundulika kuuawa na watu baada ya mwili wake kukutwa kwenye bwawa la maji.

Kamanda alisema ndugu wanaoshikiliwa ni Jumanne Kwangu, Daniel Kwangu na Emmanuel Kwangu alisema waliokiri kufanya kitendo hicho cha mauaji mtuhumiwa Mihayo Ferdinand akikiri kuchukua ng’ombe tisa ambapo wanne amewauza na kubaki na watano.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, baada ya mahojiano kuhusu mauaji ya kijana Kubeja, Agosti 8, mwaka huu, polisi wakiongozana na watuhumiwa, Emmanuel na Jumanne walienda Mpanda, Katavi kuonesha mahali walikomuua kijana huyo pori la Mlima Kasanga na kupata mabaki ya mifupa, nywele na meno na mwili.

Kamanda alisema watuhumiwa hao walikiri kutenda mauaji baada ya kuahidiwa malipo ya Sh milioni moja kwa kumuua shangazi yao na wakiwaua shangazi yao na mtoto wake na kuchukua ng’ombe wangelipwa Sh milioni 1.2.

Shuhuda wa tukio, ndugu wa waliouawa na wanaotuhumiwa, Mhoja Kishiri alisema wanaodaiwa kufanya mauaji hayo ni ndugu zao na marehemu ni shangazi yao na mwanawe.

Mke wa marehemu Kubeja, Kabula Ndalanhwa (26) alisema mtuhumiwa Jumanne alifika nyumbani kwao saa 12 jioni kumchukua mama mkwe wake akidai anaitwa na babu na mumewe alirubuniwa kwa kuelezwa kuna kazi Mpanda mkoani Katavi ndiyo hawakurudi tena. Mwenyekiti wa kijiji cha Mishepo, Mashaka Alex alisema baada ya kupewa taarifa kuna mtu yumo ndani ya bwawa la maji walifuatilia na hakujulikana alikotoka kisha wakazika.

Lakini baadaye walijitokeza ndugu baada ya kusimulia jinsi alivyokuwa na walipoona picha walimtambua kuwa ni mwenyewe na kisha kumfukua na kwenda kumzika upya kwao. Mtendaji wa Kata ya Mwantini, Goodluck Kipilimbi alisema baada ya kupewa taarifa walishirikiana na Mwenyekiti kwa kuuchunguza mwili na kuita Polisi na kuruhusiwa kuzika ukiwa umeharibika kwani ndani ya mfuko pia waliweka mawe ili azame. Diwani wa Kata ya Mwantini, Majenga Samson alidai vijana waliokamatwa walifanya mauaji.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi