loader
Picha

Magufuli ataongeza ufanisi SADC - PUMA

KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy Tanzania, imesema hatua ya Rais John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), itaongeza ufanisi na kujitanua kwa kampuni hiyo katika soko la SADC na Afrika.

Aidha, imesema kupitishwa kwa Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya SADC kutachochea fursa za kibiashara kwao na kwa kampuni nyingine za Tanzania na Watanzania kwa ujumla.

Lugha nyingine za SADC ni Kiingereza, Kifaransa na Kireno. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Dominic Dhanah, alisema hayo juzi alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa kufungwa kwa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa jumuiya hiyo akimpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na kueleza namna kampuni hiyo ilivyojipanga kuliteka soko la jumuiya hiyo katika sekta ya mafuta.

Kampuni hiyo ambayo serikali ina hisa kwa asilimia 50, ipo katika nchi 13 kati ya 16 za SADC.

Nchi ambazo haipo ni Shelisheli, Madagascar na Mauritius na imedhamiria kuzifikia nchi hizo. Dhanah alisema Tanzania ni moja ya nchi inayofanya vizuri katika soko la mafuta na vimiminika.

Hivyo kitendo cha Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti kitawaongezea nguvu ya kufanya kazi kwa wigo mpana zaidi ya ilivyo sasa.

“Puma tunampongeza Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC, lakini pia hili la Kiswahili kuwa lugha rasmi ya jumuiya ni la kupongezwa na kuungwa mkono kwani ni wazi Kiswahili kitasambaa kwa kasi na kwa kasi ya utendaji kazi wa Rais Magufuli, Puma tutazidi kufanya vizuri sokoni,” alisema Dhanah.

Alisema chini ya uongozi wa Rais Magufuli, Sera ya Viwanda imekuwa ikitekelezwa vizuri nchini Tanzania, hivyo akiwa Mwenyekiti wa SADC ana imani mkakati wa viwanda na uboreshaji wa biashara katika soko la jumuiya hiyo utakuwa wa hali ya juu na mafanikio. Dhanah alisema katika kufanikisha mkutano huo walitoa mchango kwa SADC wa Sh. milioni 300.

Awali, katika Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, Meneja wa Sheria na Uhusiano wa Puma Energy Tanzania, Goodluck Shirima, alisema katika kutekeleza sera ya serikali ya viwanda inayoendana na itifaki za SADC wameshiriki kutoa ajira kwa wananchi wa nchi wanachama.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi