loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ukosefu vibanda vya wasafiri kero Dar

UKOSEFU wa vibanda vya kujihifadhi wasafi ri wakati wa wakisubiri usafi ri wa daladala katika baadhi ya vituo jijini Dar es Salaam vimekuwa kero kubwa hasa nyakati za mvua na jua kali.

Pamoja na kwamba kwenye vituo vingi vya daladala kuna vibanda kwa ajili ya wasafiri kujihifadhi wakati wakisubiri, kuna baadhi ya maeneo vibanda havipo hali inayosababisha usumbufu na uharibifu wa mali za wasafiri kama simu na vitu vingine kunyeshewa mvua au wakati mwingine kwa kuchomwa na jua kali.

Kwa mfano, vituo vya daladala vya Magomeni Kanisani, Magomeni Mapipa, Victoria na Sayansi Kijitonyama, hakuna vibanda hivyo.

Kwa kuwa Dar es Slaam ni jiji kongwe lakini pia ni jiji kuu la kibiashara, ni vyema mamlaka husika zikaliangalia tatizo hili na kulipatia ufumbuzi wa haraka ili wananchi wanaotumia usafiri huo wajisikie salama wakati wote.

Vibanda hivyo pia ni muhimu hata kwa waenda kwa miguu ambao wakati mwingine huhitaji kupumzika kabla ya kuendelea na safari zao. Natoa mwito kwa mamlaka husika pia kuvikarabati vibanda ambavyo vimeharibika kwenye baadhi ya vituo vya daladala jijini.

Wakati mwingine maisha ya watumiaji wa vibanda hivyo yanakuwa hatarini kutokana na uchakavu au kuvunjika kwa vibanda husika. Kwa kuwa hakunawatu hulazimika kusubiri daladala wakati wamejihifadhi katika vibanda hivyo vibovu. Kero nyingine kwenye vibanda hivyo huwa ni matumizi yasiyokusudiwa yanayofanywa na wafanyabiashara ndogo ndogo wanapouza vitu.

Ni jambo la kawaida kwenye vituo vya daladala kama Makumbusho kuona wafanyabiashara hao wamepanga bidhaa zao kwenye vibanda hivyo na kufanya malengo yaliyokusudiwa ya wasafiri kujihifadhi wakati wa jua au mvua kutotimia.

Kwa vile vituo hivyo ni soko muhimu kwa wafanyabiashara ndogo, natoa mwito kwa mamlaka husika kuona njia bora ya kuwatengea maeneo wafanyabiashara hao ndani ya vituo hivyo kufanya shughuli zoa bila kuwabughudhi watumiaji waliokusudiwa wa vibanda hivyo.

Kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, anataka kulifanya Jiji hili kuwa la kisasa, matumizi yaliyokusudiwa ya kila eneo nayoyatazingatiwa kulifanya Jiji livutie zaidi.

Uboreshwaji wa miundombinu hiyo ikiwemo kujengwa kwa vituo vya kujihifadhi wasafiri kwenye vituo vya daladala ambavyo havina na kuvikarabati vilivyo vibovu, ni jambo muhimu kwa usalama na afya ya wakazi wa Jiji hili.

Naomba pia wachuuzi, wamachinga wanaouza bidhaa mbalimbali mikononi kwenye maeneo hayo, kuzingatia umuhimu wa uwepo wa vibanda hivyo kuwa ni kuwastiri abiria kituoni. Na ili kuwadhibiti Wamachinga wanaokaidi maagizo hayo, iko haja kwa vyombo vya dola kuchukua hatua kali kwa watakaokamatwa.

KATIKA miaka ya karibuni msimu wa mavuno kumekuwa na watu ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi