loader
Picha

Mbunge Gulamali ampongeza JPM uenyekiti SADC

MBUNGE wa Jimbo la Manonga lililopo Igunga mkoani Tabora Seif Gulamali amempongeza Rais John Magufuli kwa kuteuliwa wa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi zilizopo Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) pamoja na kufanikisha vyema mkutano wa SADC uliomalizika Jumapili Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari Gulamali pamoja na mambo mengine pia alimpongeza Rais Magufuli na watanzania wote kutokana na lugha ya Kiswahili kuchaguliwa kuwa moja ya lugha itakayotumiwa katika mikutano ya SADC, suala alilosema litazidi kulitangaza taifa la Tanzania.

Alisema kitendo cha Rais Magufuli kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC katika mkutano huo huo kunazidi kuiletea heshima Tanzania ambayo tangu ilipoapata uhuru wake Mwaka 1961 imeendelea kuwa kitovu kikuu cha Amani miongoni mwa Mataifa mbalimbali katika Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.

Aidha alisema pamoja na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC pia mkutano huo wa wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo ulifana chini ya Uenyeji wake huku hotuba yake ikigusia maeneo muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya Jumuiya hiyo na Wananchi wake, jambo alilodai kuwa litazidi kuhimarisha Umoja na mshikamano wa Nchi hizo kama alivyokuwa ameligusia katika hotuba yake alipokuwa akifunga mkutano huo.

Alisema kauli ya Rais Magufuli kusema kuwa Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika kwa wanachama wa SADC ili kuharakisha jitihada za kuleta maendeleo fungamani, linaonyesha ni kwa namna gani Kiongozi huyo ana kiu ya kuziona nchi zote zilizomo ndani ya SADC zinapiga hatua zaidi za kimaendeleo kama alivyo na kiu hiyo kwa Tanzania .

“Pamoja na kuzitaka nchi Wanachama kutoa kipaumbele katika suala zima la Usalama, Amani na Utulivu pia alizitaka kuboresha eneo la ukuaji wa Viwanda, Biashara na utengenezaji wa fursa za kibiashara, jambo ambalo ni muhimu katika uzalishaji wa Ajira na Maendeleo yake na Wananchi kwa ujumla, anastahili pongezi kwa kuliona hili”alisema Gulamali.

Alisema kimsingi mambo mengi ambayo Rais Magufuli amegusia katika hotuba yake hiyo yana akisi yale anayoendelea kuyafanya hapa nchini ambayo kwa kiasi kikubwa matokeo yake yanaonekana kwa kadri siku zinavyozidi kwenda huku akitoa rai kwa Mataifa Wanachama wa SADC kuyatekeleza ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa.

Gulamali alisema hatua ya Rais Magufuli kuzitaka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kuweka mkazo katika usimamizi wa rasimali zake una maana kubwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama ambapo pato lake la ukuaji wa uchumi kwa Taifa ni wastani wa asilimia 22 katika kipindi cha Mwaka 2018.

Aidha kuhusu lugha ya Kiswahili kuchaguliwa kuwa miongoni lugha ya nne za kimataifa kutumika katika mikutano ya SADC, ni fahari kwa Tanzania kwa kuwa itazidi kulitangaza Taifa na kuzidi kuliletea heshima katika Mataifa mbalimbali huku tayari lugha hiyo ikitajwa kuzungumzwa katika mataifa 10 Duniani.

Aliwataka watanzania kutumia fursa hiyo adhimu ya kutumika kwa lugha hiyo kwenda kutafuta fursa mbalimbali katika Mataifa hayo ili kuzidi kukitangaza pamoja na kujiingizia kipato kutokana na Ajira zitakazoendelea kutolewa ndani ya nchi hizo.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi