loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wapenzi mbaroni kwa kuchukua mchanga ufukweni

Wapenzi raia wa Ufaransa wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 6 nchini Italia baada ya kukutwa na hatia ya kuchukua mchanga kwenye visiwa vya Sardinia walikokuwa wamekwenda kwa mapumziko.

Inadaiwa kuwa mchanga wa visiwa hivyo unalindwa na ni kosa kisheria kuondoka nao, hivyo wapenzi hao walivunja sheria kwa kuubeba mchanga huo warudi nao nyumbani Ufaransa kama ukumbusho.

Inaelezwa kwa polisi kwenye mji wa Porto Torres waliukuta mchanga huo kwenye gari la wapenzi hao wakati wakipita kwenye ukaguzi wa magari, hivyo wakakamatwa.

Wapenzi hao wamedai kuwa, hawakujua kwamba ni kosa kisheria kuondoka na mchanga huo.

Kuna taarifa kwamba, baadhi ya watalii nchini Italia wanaokwenda kwenye visiwa wanajikuta kwenye mikono ya sheria na kulazimika kulipa faini au kufungwa jela kwa sababu ya kuondoka na mchanga wa ufukweni.

RAIS wa Urusi, Vladimir ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Post your comments