loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Staa wa "Hobbs & Shaw" aaga ubachela

Mwigizaji wa Hollywood Dwayne Johnson maarufu kama "The Rock" ameaga ubachela kwa mara ya pili sasa, baada ya kutangaza kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Lauren Hashian.

The Rock aliweka picha yake na mkewe huyo kwenye mtandao wa Instagram wakiwa visiwani Hawaii, wakionyesha kufurahia na kuandika maelezo yaliyoonyesha kuwa wamefunga ndoa.

Staa huyo mwenye miaka 47, na Hashian, 34, ni wazazi wa watoto wawili Jasmine, 3, na Tiana, 1.

Ana mtoto wa kwanza mwenye umri wa miaka 18 ambaye alizaa na mkewe wa kwanza Garcia.

Wawili hao walikutana mwaka 2006, wakaanzisha uhusiano mwaka 2007 mara baada ya Johnson kutalakiana na mkewe Garcia.

RAIS wa Urusi, Vladimir ...

foto
Mwandishi: Mashirika

Post your comments