loader
Picha

Usajili NGOs mwisho Agosti 30

MASHIRIKA yasiyo ya kiserikali (NGOs) ambayo hayatakuwa yamefanya usajili wake kwa mujibu wa sheria hadi kufikia Agosti 30, mwaka huu, yatakuwa yamejifuta yenyewe Msajili wa NGOs, Vickness Mayao aalisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu fursa ya mwisho ya kujisajili.

Alisema baada ya marekebisho ya Sheria ya NGOs Namba 24 ya Mwaka 2002, serikali ilitoa miezi miwili kuanzia Julai 10 hadi Agosti 30, mwaka huu, mashirika kusajili kwa sheria yake.

Kwa mujibu wa Sheria ya NGOs Namba 24 ya Mwaka 2002 iliyorekebishwa chini ya Sheria Namba 3 ya Mwaka 2019, mashirika yanayotakiwa kusajiliwa ni yanayoendesha shughuli za kijamii, kiutamaduni, kiuchumi, utawala bora, haki za binadamu na mazingira katika ngazi ya jamii ambayo shughuli zake hazijalenga kugawana faida au kukuza biashara.

Sheria imeweka wazi muda ukiisha kila shirika linatakiwa kuwa limejisajili kwenye sheria inayolihusu, bila hivyo watakuwa wamejifuta. Mayao alisema tangu kufungua usajili Julai 10, 2019, wamefanya usajili wa NGOs kanda tano.

“Tumefanya utaratibu wa kusajili NGOs kanda tano, na tumerudi Dodoma kuanzia kesho hadi Agosti 27, mwaka huu, ndio mwisho, “ alisema.

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amesema kama Rais John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi