loader
Picha

'Watanzania kaoneni maajabu maporomoko Kalambo'

Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imesema msitu wa Kalambo umepandishwa hadhi ili maporomoko ya Mto Kalambo yahifadhiwe na kusimamiwa.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy ameyasema hayo akiwa kwenye Msitu wa Hifadhi ya Mazingira asili ya Kalambo ikiwa ni sehemu ya ziara kutembelea maeneo ya hifadhi za misitu na mashamba ya miti ya Serikali.

Ametoa mwito kwa Watanzania waanze kuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi hiyo kujionea maajabu ya maporomoko hayo.

“Eneo hili linavutia na zuri kwa utalii, nitoe wito kwa Watanzania wakiwa katika siku za mapumziko na sikukuu kutembelea na kushuhudia maajabu ya maporomoko haya ambayo yameshatangazwa na Shirika la Umoja wa Matifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (Unesco) kuwa ni urithi wa dunia.”amesema Brigedia Jenerali Mkeremy.

“Niwapongeze TFS kwa ujenzi wa ngazi zenye urefu wa mita 1,277 zinazoshuka hadi kwenye maporomoko haya yanayomwaga maji Ziwa Tanganyika. Nimeambiwa kuwa katika ngazi za kushuka chini kwenye maji kuna “view point” tatu, ya kwanza unapotoka kwenye maji imepewa jina la Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii “Kigwangala view point” napendekeza katika “view point” ya pili ambayo ni ya kwanza unapoteremka ngazi iitwe Dos Santos View point, na ya tatu inayofuatia iitwe, “Mkeremy view point,” amesema.

Kamishna Mhifadhi wa Misitu Profesa Dos Santos Silayo amesema TFS imeweka mikakati kuhakikisha misitu inaingiza mapato ya kutosha kupitia utalii na kuuza mazao ya misitu.

Ametaja miongoni mwa mikakati hiyo ni kuvitangaza vivutio vya utalii ekolojia vilivyopo kwenye misitu ya mazingira asilia iliyo chini ya taasisi hiyo.

“Utalii ekolojia na biashara ya mazao ya misitu na nyuki ni nguzo ya utendaji kazi wa taasisi yetu, tunafanya kila liwezekanalo kuimarisha maeneo ya Maporomoko ya Kalambo ili yaweze kutusaidia kuongeza tija katika jukumu letu la ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali, kuongeza mauzo ya nje na fedha za kigeni kupitia huduma za utalii na uuzaji wa mazao ya nyuki,” amesema Profesa Silayo.

Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed (CUF) amejiuzulu kiti ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi