loader
Picha

'Wanawake onesheni uwezo muwe viongozi'

IDARA ya Habari (MAELEZO) imewataka wadau wa habari kufanya utafiti kuhusu masuala ya kijinsia katika vyombo vya habari na imehimiza wanawake wajiamini na kuonesha uwezo wanapopata nafasi za uongozi.

Mkurugenzi Msaidizi wa idara hiyo, Rodney Thadeus ameyasema hayo anafungua mafunzo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma kuhusu usawa wa kijinsia kwenye vyombo vya habari.

Mafunzo hayo yanatolewa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa) kwa ufadhili wa Taasisi ya Maendeleo na Vyombo vya Habari Finland (Vikes).

Thadeus amesema kwa sasa kwenye vyombo vya habari wanauume wamekuwa wengi ukilinganisha na wanawake sambamba na suala la waliopewa uongozi ndani ya vyombo hivyo.

“Tunamaliza kwenye vyuo lakini tukija kwenye vyumba vya habari wanaume ndio wengi kuliko wanawake, lakini pia hata linapokuja suala la uongozi bado idadi kubwa ni wanaume, sasa ili kuja na suluhisho la kudumu ni vema tukafanya utafiti wa kina,” amesema Thadeus.

Ametoa mwito kwa wanawake wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari kujiamini na kuonesha uwezo ili waaminiwe na kupewa nafasi za uongozi.

Amesema wanawake wana uwezo mkubwa hivyo wanatakiwa kujiamini na kujifunza zaidi hasa ikizingatiwa kuwa hata Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanahimiza usawa wa kijinsia.

“Mjijengee kujiamini na kufanya kazi katika ubora unaotakiwa mnaweza kufikia nafasi za juu za uongozi ambazo zinashikwa na wanaume kwenye vyombo vyenu vya habari,” amesema.

Amesisitiza haja ya waandishi wa habari kujiendeleza kimasomo ili kuongeza maarifa na kukidhi matakwa ya Sheria ya Huduma kwa Vyombo vya Habari ambayo imeweka kiwango cha elimu angalau Stashahada ya Uandishi wa Habari.

“Pia dunia imebadilika haipo ardhini lazima tujikite kwenye mitandao ya kijamii msibaki kwenye magazeti tu mjikite na huko,” amesema.

Pia, Thadeus amewaasa kutumia mitandao ya kijamii bila kupotosha na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.

“Kuna shida sana sasa hivi kwenye masuala ya mitandao ya kijamii na utangazaji, yaani ukisikiliza redio unasema nini hiki matumizi ya lugha hovyo, vichwa vya habari kwenye mitandao ya kijamii vya ajabu, najua ni kwa sababu vinawekwa na wanaume, wanawake mnaweza kubadili hii hali,” alisema.

Ametumia fursa hiyo kupongeza vyombo vya habari kutokana na kazi nzuri vinavyoifanya wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na kutaka ushirikiano huo uendelee hata wakati wa Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki litalifanyika mwezi ujao.

Mkurugenzi wa Tamwa, Rose Reuben alisema wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi kwenye vyombo vya habari ikilinganishwa na wanaume.

DAKTARI aliyetajwa na Rais John Magufuli, kumtibu akiwa naibu waziri ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi