loader
Picha

Balozi za Tanzania kutafuta masoko

WIZARA ya Viwanda na Biashara imepanga mkakati wa kuweka watu mahususi wa kutafuta masoko katika balozi za nchi, zinazonunua kwa wingi mazao ya Tanzania, kwa lengo la kurahisisha na kuharakisha uuzaji wa bidhaa nje ya nchi.

Waziri wa wizara hiyo, Innocent Bashungwa amesema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kikao cha ndani kati ya mabalozi wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi, kilichoandaliwa na wizara yake na ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Bashungwa ambaye hakutaja nchi zinazonunua bidhaa za Tanzania kwa wingi, ambazo wanaweza kuanzia mkakati huo, alisema suala hilo ni miongoni mwa ambayo aliliwasilisha kwenye kikao hicho ambacho mjadala uliendelea kabla ya kufikia hitimisho.

“Nchi ziko nyingi...kwenye mjadala tutajadiliana na baada ya hapo tutakubaliana kulingana na bajeti. Labda tunaweza kwenda taratibu lakini mkakati ni kuhakikisha nchi nyingi hasa hasa zinazonunua bidhaa nyingi zinakuwa na hawa maofisa wa biashara,” amesema.

Alisema mtu huyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambayo iko chini ya wizara yake, ataweza kufanya uratibu mzuri kuhakikisha bidhaa zinazokwenda nje ya nchi zinapokewa na ofisa mwenye utaalamu.

"Hiyo ndiyo namna bora ya kutumia diplomasia ya kiuchumi kuhakikisha bidhaa kupitia balozi za nje zinapata masoko"amesema.

Alisema moja ya mkakati ni kuhakikisha balozi zinatumika kuhakikisha wakulima wanapata masoko ya uhakika.

Akizungumzia kikao cha jana, amesema awali walitaka kutumia njia ya video kujadiliana na mabalozi walioko nje kujadiliana suala zima la ushiriki wao katika azma ya serikali ya kutumia diplomasia ya uchumi kutafuta masoko.

“Matarajio yetu kutoka kwa mabalozi ni kufanya kama wanavyofanya mabalozi wa nchi zinazoendelea wanaojenga uhusiano kwa ajili ya kampuni za nchini kwao,” amesema Bashungwa.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi