loader
Picha

Dhahabu kusafishwa Dodoma, BOT kuinunua

Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa na kiwanda cha kuchenjua na kusafisha dhahabu kinachotarajiwa kuanza kazi Oktoba mwaka huu.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Madini, Doto Biteko baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kitakachochenjua na kusafisha dhahabu kwa asilimia 99.9.

Amesema mbali na kusaidia wafanyabiashara nchini katika kuchenjua na kusafisha dhahabu zao, pia uwepo wa kiwanda hicho utawezesha nchi kuwa na akiba ya madini hayo yatakayonunuliwa na Benki ya Kuu (BoT).

Januari mwaka huu, Rais John Magufuli aliagiza BoT kuwa na akiba ya dhahabu na kuhimiza haja ya serikali kudhibiti usafirishaji wa madini kutokana hapa nchini ambayo ni nchi ya nne kwa kuzalisha dhahabu.

“Tunatakiwa kuanza kununua dhahabu, BoT inatakiwa kuwekeza kwenye hili. Tunatakiwa kuwa na akiba yetu si tu kwenye dola bali hata kwenye dhahabu, kwa sababu dhahabu ni fedha,” amesema Rais Magufuli.

Biteko amesema kuanzia Oktoba mwaka huu, BoT itaanza kununua dhahabu iliyosafishwa ambayo itaweka kwenye “akiba ya Taifa ya dhahabu’ na hatimaye kusaidia nchi kuuza dhahabu na kushindana kwenye soko la kimataifa.

Amesema hatua ya kuanzisha kiwanda cha kuchenjua na kusafisha dhahabu nchini ni takwa la kisheria kutokana na mabadiliko ya hivi karibuni ya Sheria ya Madini, na kuongeza kuwa mpaka sasa tayari serikali imetoa leseni mbili za kuanzisha kiwanda cha kusafisha dhahabu mkoani Dodoma na Mwanza.

Amesema walijitokeza jumla ya waombaji 24 na waliopewa vibali wa uendeshaji wa shughuli za kurefine na ku-smelte ni sita.

“Kati ya viwanda hivyo sita vitakavyojengwa nchini viwanda viwili ni vya kurefined madini ya dhahabu, copper na silver ambavyo vipo katika mikoa ya Dodoma na Geita,” amesema na kuongeza kuwa viwanda vinne vya Smelter ambavyo vimejengwa Kyerwa mkoani Kagera, Mpwapwa (Dodoma) na Kahama (Shinyanga).

Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Ferenc Milnar alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho uliogharimu dola za Marekani milioni 2, umekamilika kwa asilimia 75 na kwamba hivi sasa wanasubiri vifaa kutoka nchini Italia.

Alisema baada ya kufika vifaa hivyo nchini mwezi ujao, watatumia siku saba kuvifunga. Molnar pia alimuhakikishia waziri kuwa watahakikisha kiwanda hicho ndani ya muda uliopangwa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha hicho, Prince Mugisha alisema wataanza kwa usafishaji wa mfano ambao utakuwa kilo 30 hadi 50 kwa siku. Alisema mwakani watakuwa wakisafirisha kilo 1,000 kwa siku.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema utekelezaji wa sehemu wa Sheria ya Madini inayotaka theluthi moja ya mrahaba utolewe kama dhahabu utaanza kutekelezwa mara baada ya kiwanda cha uchenjuaji wa dhahabu cha kwanza kukamilika kati ya Oktoba.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge aliwahakikisha wawekezaji wanaotaka kuwekeza mkoani humo kuwa watapata msaada unaotakiwa na kufika ofisini kwake kama wanakumbana na urasimu wa aina yoyote.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi