loader
Picha

Kampeni ya 'Elimisha Kibaha' kujenga madarasa 30

WILAYA ya Kibaha mkoani Pwani inatarajia kujenga vyumba vya madarasa 30 kati ya 65 vinavyohitajika kupitia kampeni ya Elimisha Kibaha inayolenga kuunga mkono ya sera ya elimu bila malipo kwa shule za sekondari na msingi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Jumatano, huku akiongeza kuwa fedha zitakazopatikana kupitia kampeni hiyo zitatumika kununua viti 3,250 na meza 3,250.

Mshama alisema kuwa halmashauri mbili za Kibaha Mji na wilaya ya Kibaha zina mapungufu ya madarasa 65 kwa shule za sekondari ambapo upungufu wa madarasa umetokana na ongezeko la wanafunzi wanaofaulu.

“Kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaofaulu ambapo kwa mwaka 2017 jumla ya wanafunzi 3,560 walifaulu, mwaka 2018 wanafunzi 3,938 na mwaka 2019 wanafunzi waliongezeka na kufika 4,930 hali ambayo imesababisha madarasa kuwa pungufu,” alisema Mshama.

BODI ya Ithibati inayotajwa katika Sheria ya Huduma ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi