loader
Picha

Yanga- Hatuna tatizo na Zahera

UONGOZI wa mabingwa wa kihistoria, Yanga umesema hauna tatizo lolote na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha wao mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten ikiwa ni siku moja baada ya Kocha Zahera kudai kambi waliyoweka Kilimanjaro na Arusha kujiandaa na mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers haikuwa na manufaa kwa kikosi chao.

Ten alisema kocha wao alizungumza vizuri lakini anaamini kwamba maneno hayo aliyatoa akiwa na presha ya mchezo kwani ratiba ya kwenda kuweka kambi hiyo ilifanyika kwa kutekeleza majukumu yaliyotolewa na benchi la ufundi la kikosi hicho.

“Hatuna tatizo lolote na kocha Zahera, lakini tunaamini alizungumza maneno hayo kutokana na presha ya mechi, siwezi kuamini kama uongozi unaweza kuratibu michezo ya kirafiki nje ya benchi la ufundi,” amesema Ten.

Alisema baada ya kumalizika mchezo wa awali dhidi ya Township Rollers benchi la ufundi liliomba mechi mbili za kirafiki ikiwa mechi moja ya ndani na nyingine ya kimataifa jambo ambalo uongozi ulilitimiza.

Alisema wao kama uongozi wanaamini kupitia mechi hizo za kirafiki timu itakuwa imesoma na imejifunza kitu kipya ambacho kitakuwa na faida kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Rollers.

Wakati huohuo kikosi cha mabingwa hao tayari kipo Gaborone Botwana kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii.

Katika hatua nyingine, kocha wa Polisi Tanzania Selemani Matola ameitabiria timu hiyo kufanya vizuri katika mechi hiyo kwani tayari imeshajifunza katika mechi zilizopita.

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi