loader
Picha

Warembo 20 kuwania taji Miss Tanzania

FAINALI za Miss Tanzania 2019 zinatarajiwa kufanyika keshokutwa kwenye ukumbi wa New Millennium Towers LAPF uliopo Makumbusho Dar es Salaam. Warembo 20 kutoka mikoa ya Tanzania wapo kambini tangu Agosti 12 wakijiandaa na kinyang’anyiro hicho.

Wakiwa kambini warembo hao wameshiriki katika shughuli za kijamii, ikiwa ni kutembelea katika kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi mwisho Dar es Salaam.

Wakiwa katika kituo hicho warembo waliwafariji watoto kwa kucheza nao michezo ya aina mbalimbali na kula nao chakula pamoja.

Warembo hao pia walishiriki kwenye shindano la kumsaka Mrembo mwenye kipaji, mrembo mwenye mvuto katika picha, mrembo mwanamitindo, mrembo mwanamichezo na mrembo chaguo la watu.

Warembo hao wapo ambao wameingia katika hatua ya tano bora na washindi katika mashindano hayo watatangazwa katika fainali hizo keshokutwa.

Akizungumza jana Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look ambayo ndio waandaji wa shindano hilo, Basila Mwanukuzi alisema maandalizi yote yameshakamilika na kinachosubiriwa ni tukio lenyewe.

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi