loader
Picha

Manara- Mashabiki wachezaji muhimu Simba

IKOSI cha Simba kimeingia kambini jana tayari kujifua na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya UD Songo inayotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumapili ya wiki hii.

Katika mechi hiyo ya raundi ya awali, Simba inahitaji ushindi kusonga mbele baada ya kutoka suluhu ugenini Beira, Msumbiji wiki mbili zilizopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara alisema maandalizi ya mchezo huo yanaenda sawa na kikosi cha timu hiyo kimeshaingia kambini.

“Maandalizi yanaendelea vizuri kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mechi yetu ya kimataifa,dhidi ya Songo, kikosi kimeshaingia kambini,tunawaomba mashabiki wajitokeze uwanjani kuwaunga mkono wachezaji kuhakikisha tunapata ushindi,” alisema Manara.

“Sisi kwetu shabiki sio mchezaji wa 12 tu uwanjani, bali ni mchezaji muhimu kwenye kila idara, tunawaomba mashabiki wetu na wanachama twendeni Taifa Jumapili tukaujaze uwanja.”

Aidha, Manara amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuziunga mkono na timu nyingine zinazoiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo ya kimataifa kwa kujitokeza kwa wingi kuwashangilia.

Timu nyingine zinazoshiriki michuano ya kimataifa mwishoni mwa wiki hii mbali na Simba ni Yanga, itakayokuwa ugenini kucheza na Township Rollers kwneye mechi ya Ligi ya Mabingwa, na Azam na KMC zinazocheza kombe la Shirikisho zitamenyana na Fasili Ketema ya Ethiopia na AS Kigali ya Rwanda.

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi