loader
Picha

Manula: Nilihama Azam kufuata maslahi

KIPA wa Simba SC na timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’, Aishi Manula amesema alihama Azam kufuata maslahi kwa sababu hakutaka mwajiri wake wa zamani apunguze maslahi yake.

Amesema jijini Dar es Salaam kuwa, wakati huo, Azam FC walikuwa kwenye kipindi cha mabadiliko ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji.

“Kwa hiyo walikuwa wanataka kubana matumizi, hivyo kuna baadhi ya vitu, yaani vifinywefinywe ili matumizi yale yabadilike…kwa hiyo kama ulikuwa unapata laki tano wanakwambia kwa sababu klabu inabana bajeti, ina maana wanataka kukupa labda laki mbili au tatu, kwa hiyo kama fedha za usajili ni elfu mbili kwa sababu wanataka kubana matumizi utapata mia tano,” amesema kwenye mahojiano katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Amesema, yeye ni miongoni mwa waliokataa mabadiliko hayo kwa sababu alizingatia kuwa hana muda mrefu wa kucheza soka hivyo maslahi mazuri kwake ni jambo muhimu.

“Lifespan (muda wa kucheza) yetu kwenye mpira sio zaidi ya miaka kumi na tano kwa hiyo kuna kipindi unafika unajiona kabisa mimi nastahili kupata fedha kiwango hiki,”amesema kijana huyo shabiki wa Chelsea ya England.

Manula amesema, kabla ya kuhamia Simba hakuwahi kuwa shabiki wa timu hiyo ila alikuwa na ndoto za kuichezea.

Amesema pia miaka ya nyuma hakuwahi kuwa shabiki mkubwa wa timu yoyote, hakuwa anafuatilia soka ila alipenda zaidi kuucheza mchezo huo.

Kijana huyo amesema, wakati anaanza kujifunza soka hakuwa anacheza nafasi ya kipa na hadi sasa ana uwezo wa kucheza nafasi za ndani.

Amesema awali alikuwa anacheza beki namba mbili, namba tatu, lakini baadaye akamudu zaidi kucheza nafasi za ushambuliaji hasa winga, namba tisa na 10.

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema hajaridhishwa na ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi