loader
Picha

Magufuli apongezwa kuongoza SADC, Kiswahili

MBUNGE wa Manonga wilayani Igunga, Tabora, Seif Gulamali, amempongeza Rais John Magufuli kwa kushika wadhifa wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kufanikisha mkutano wa jumuiya hiyo uliomalizika Jumapili jijini Dar es Salaam.

Gulamali pia amempongeza Rais Magufuli na Watanzania kutokana na Kiswahili kuchaguliwa kuwa moja ya lugha itakayotumiwa katika mikutano ya SADC, suala alilosema litazidi kuitangaza vyema Tanzania.

Alisema kitendo cha Rais Magufuli kushika wadhifa huo wa Mwenyekiti wa SADC katika mkutano huo kinazidi kuiletea heshima Tanzania ambayo tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1961 imeendelea kuwa kitovu kikuu cha amani miongoni mwa mataifa mbali mbali katika Bara la Afrika na dunia kwa ujumla.

Alisema mkutano huo wa wakuu wa nchi za SADC ulifana chini ya uenyeji wa Rais Magufuli, huku hotuba yake ikigusia maeneo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya jumuiya na wananchi wake, jambo alilosema litazidi kuimarisha umoja na mshikamano wa SADC kama alivyogusia katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa 39 wa jumuiya hiyo yenye nchi 16.

Gulamali alisema kauli ya Rais Magufuli kusema Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika kwa wanachama wa SADC ili kuharakisha jitihada za kuleta maendeleo fungamani, linaonesha ni kwa namna gani ana kiu ya kuziona nchi zote zilizomo ndani ya SADC zinapiga hatua zaidi za kimaendeleo kama alivyo na kiu hiyo kwa Tanzania.

DAKTARI aliyetajwa na Rais John Magufuli, kumtibu akiwa naibu waziri ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi