loader
Picha

RC ataka ufumbuzi changamoto za mipaka

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amewataka wajumbe wanaoshiriki kikao cha uimarishaji wa mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya kutumia kikao hicho kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa changamoto za mipaka badala ya kushindana.

Gambo ametoa rai hiyo  jijini hapa wakati akifungua kikao cha mwendelezo wa uimarishaji mipaka ya kimataifa baina ya Tanzania na Kenya.

Amesema utatuzi wa changamoto za mipaka ya kimataifa kati ya Kenya na Tanzania unafanywa na nchi husika bila kushirikisha mataifa ya nje na kueleza kwamba hiyo inaonesha ni jinsi gani nchi hizo zinavyoweza kukaa pamoja kwa kujiamini na kupata ufumbuzi wa masuala yao.

Ametoa rai kwa wajumbe wa kikao cha nchi hizo mbili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za mipaka ya kimataifa kwa kukubaliana na kuzingatia tamaduni za nchi hizo pamoja na miongozo ya viongozi wa nchi husika.

Amewataka washiriki kudumisha pia mahusiano ya kijamii wakati wa majadiliano yao kwani wananchi wanaoishi mipakani wana mahusiano mazuri ya kindugu na kusisitiza kuwa hali hiyo itadumisha umoja na mshikamano uliopo kati ya nchi hizo.

Awali, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mathias Kabundugulu, amesema kikao hicho cha siku tano ni mwendelezo wa vikao vya uimarishaji mipaka ya kimataifa katika maeneo mbalimbali ya mipakani ikiwa na lengo la kuondoa changamoto kama ilivyoelekezwa na Umoja wa Afrika (AU).

Kwa mujibu wa Kabundugulu, kikao hicho kitapokea taarifa ya ukaguzi wa kipande cha mpaka cha kilometa 128 kutoka eneo la Ziwa Natron hadi Namanga mkoani Arusha, lengo likiwa ni kuimarisha mpaka huo hadi Tarakea mkoani Kilimanjaro na baadaye Jasini mkoani Tanga.

WATOTO yatima na wanaoishi kwenye mazingira wa magumu wa shule ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi