loader
Picha

Mkurugenzi kizimbani mashitaka 50

MKURUGENZI Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Ester Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka 50 likiwemo la kughushi, ubadhirifu, na kutumia nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya mwajiri wake.

Mbali na Liwa, mshitakiwa mwengine ni dereva wa wizara hiyo, Johansen Kaimukirwa aliyefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka manane ya kughushi na kutoa nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya mwajiri wake.

Akisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo, Wakili wa Serikali Paschal Magabe, amedai kuwa Liwa alitenda makosa hayo kati ya Machi 11 na Juni 30, 2015 katika ofisi za wizara hiyo.

Amedai kuwa, katika mashitaka ya kwanza hadi ya 16, kwa nia ovu alighushi nyaraka yenye kichwa cha habari "Posho ya kujikimu” kwa maofisa wa wilaya 16 ambapo kila mmoja alilipwa Sh 32,500 kama posho ya kuhudhuria mafunzo ya uhamasishaji kwa vijana yaliyofanyika mkoani Singida.

Katika mashitaka ya 17 hadi 20, mshitakiwa huyo anadaiwa kughushi nyaraka yenye kichwa cha habari “Posho ya Waandishi wa habari” alionesha kuwa Festo Sanga wa Kituo cha Redio cha Standard Fm, amelipwa jumla ya Sh 1,030,000 na Emmanuel Michael Sh 100,000 kama malipo ya kuhudhuria mafunzo hayo.

Liwa anadaiwa kuwa kughushi hati ya malipo ya jumla ya Sh 405,000 akionesha maduka ya vifaa vya ofisi ya Mwaji na Temo yalilipwa kiasi hicho cha fedha kama gharama ya vifaa vilivyotumika katika mafunzo hayo. Wakili huyo wa serikali alidai, Juni 25 mwaka 2015, Liwa akiwa ofisi za Wizara ya Habari, alitumia nyaraka za kughushi akionesha Sh 11,177,000 zilitumika katika kipindi cha mafunzo hayo ya vijana mkoani Singida.

Ilidaiwa kuwa kati ya Machi 11 hadi Juni 30, 2015, mshitakiwa huyo alifanya ubadhirifu na ufujaji wa Sh 5,425,000 alizokabidhiwa na wizara hiyo kwa lengo la kufanya mafunzo hayo mkoani Singida.

Mshitakiwa alikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtega, Wakili wa Serikali Joseph Kiula alidai Liwa alighushi nyaraka kuonesha kwamba watu 18 walihudhuria mafunzo ya uhamasishaji kwa vijana Mkoa wa Ruvuma na 17 kati yao walilipwa Sh 32,500 na mmoja alilipwa Sh 65,000.

Pia alighushi nyaraka kuonesha kuwa Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Hamza Mashore alilipwa Sh 750,000 kama posho ya kazi za uandaaji wa habari na DVD.

Liwa anadaiwa alighushi risiti kuonesha kuwa Sh 400,000 zililipwa kwa duka la vifaa vya ofisi la Majestic T Ltd kununua vifaa vilivyotumika kwenye mafunzo hayo.

Inadaiwa Septemba 23, 2015 Liwa akiwa wizarani alitumia nyaraka ya uongo kumuonesha mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kuonesha ni marejesho ya masurufu maalumu kuonesha alitumia Sh 10,325,000 katika mafunzo hayo.

Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed (CUF) amejiuzulu kiti ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi