loader
Picha

Kiwanda Songwe kuuza chumvi SADC

UONGOZI wa Kiwanda cha Chumvi cha Itumbula katika Kata ya Ivuna wilayani Momba Mkoa wa Songwe, umesema utaanza uzalishaji mwishoni mwa mwezi huu ambapo chumvi yake itasambazwa ndani na nje ya nchi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili kuongeza mapato ya halmashauri hiyo, mkoa na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwenye ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkuu wa mkoa huo, Nicodemas Mwangela alisema kiwanda hicho kitaanza kuzalisha rasmi chumvi mwishoni mwa mwezi huu.

Mwangela alisema mradi huo wa uzalishaji chumvi unategemewa kuwa mkubwa ambao utazalisha chumvi ambayo itatumika ndani ya Mkoa wa Songwe, ndani ya Taifa na katika nchi jirani hasa za kusini mwa Afrika.

“Mradi huu wa chumvi kuna uwezekano ukawa mkubwa kuliko hata ule wa Uvinza (Kigoma), soko la uhakika kwa upande wa chumvi lipo ndani ya nchi yetu na nyingine tutaziuzia nchi za kusini mwa Afrika zilizopo kwenye Jumuiya ya SADC,” amesema Mwangela.

“Tarehe 22 mwezi huu (kesho) chumvi itakuwa tayari na nitakuja kuchukua baadhi ya paketi za kwanza kwa ajili ya matumizi yangu na viongozi hawa wa Kamati ya Siasa Mkoa,” amesema.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe, Elniko Mkolla alisema ahadi za chama tawala ilikuwa ni pamoja na kutengeneza ajira kwa vijana hivyo anategemea vijana wengi watapata ajira kupitia mradi huo.

Pia aliiagiza Serikali ya Mkoa kutatua baadhi ya changamoto zilizopo katika kiwanda hicho ikiwamo changamoto ya miundombinu ya barabara ili mradi uanze haraka na kunufaisha wakazi wa Momba na nchi kwa ujumla. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Adrian Jungu alisema mradi huo mpaka kukamilika utagharimu Sh milioni 535 utakuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya tani 50 mpaka 60 kwa mwaka. “Mradi huu utakuwa na manufaa makubwa sana kwa halmashauri yangu kwa sababu mapato yataongezeka, lakini pia vijana zaidi ya 4,000 watapata ajira katika kiwanda hiki cha chumvi,” alisema Jungu.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara ...

foto
Mwandishi: Baraka Messa, Songwe

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi