loader
Picha

Kilo kakao sh 5,000/- Morogoro

BEI ya kakao kavu kutoka kwa wakulima wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro imeongezeka kutoka wastani wa kilo moja Sh 2,000 hadi 2,500 msimu uliopita hadi Sh 3,500 hadi 5,000 mwaka huu.

Ofisa Kilimo wa Kata ya Mbingu wilayani Kilombero, Ally Mohamed Mula amesema hayo hivi karibuni mjini Morogoro alipozungumza na gazeti hili juu ya mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la kakao katika kata hiyo na maeneo mengine ya wilaya yenye kustawi kwa zao hilo jipya ndani ya Wilaya ya Kilombero.

Zao la kakao linalimwa zaidi na wakulima wa vijiji vya Kata ya Mchombe, Mbingu na Mngeta katika Tarafa ya Mngeta, na ni zao jingine la kibiashara licha ya mpunga ambao ambalo pia ni la chakula wilayani humo.

Mula amesema wilaya hiyo ina wakulima zaidi ya 2,600 wanaozalisha zao la kokoa na wengi wao ni kutoka katika ukanda wa vijiji hivyo vitatu ambao kwa msimu uliopita uzalishaji kiwilaya ulikuwa ni tani 358 za kokoa kavu.

Amesema uzalishaji wa kilimo cha kokoa katika maeneo hayo umekuwa uliongezeka kutokana na wakulima kuona hilo ni zao litakalowaongezea kipato kiuchumi kitakachowasaidia kuleta maendeleo yao na familia zao.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi