loader
Picha

Ashikwa na paketi 68 za 'cocaine' tumboni

Raia wa Kenya Glenn Chibasellow Ooko anashikiliwa na jeshi la polisi nchini Thailand baada ya kukamatwa na pakiti 68 za dawa za kulevya aina ya cocaine tumboni mwake.

Tukio hili lilitokea jana, Jumatano katika uwanja wa ndege wa Bangkok alipowasili akiwa anatokea nchini Ethiopia.

Inaelezwa kuwa Ooko ambaye ana umri wa miaka 43, alikuwa amemeza paketi hizo 68 zilizokuwa na uzito wa kilogramu 12.

Jeshi la polisi nchini humo linamshikilia Osita Joseph Ukpa, raia wa Nigeria ambaye anasadikika kuwa mwajiri wa Ooko kwenye kusafirisha dawa za kulevya.

Mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert ...

foto
Mwandishi: Na Mashirika

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi